NAFASI YA KILIMO NA SERA ZAKE KATIKA KUFANIKISHA TANZANIA YA VIWANDA

SHARE:

TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imefanya mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ...

TAASISI ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imefanya mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara.
Katika mhadhara huo msemaji Mkuu alikuwa Prof. Brian Van Arkadie, majadiliano yalitanguliwa Prof Samuel Wangwe na Aloyce Hepelwa
Akiwasilisha mada yake aliwataka wataalamu kubadilika katika namna ya kusaidia kuongeza tija katika kilimo na kuachana na dhana za zamani kwamba wakulima wameshindwa kubadilika na kukwamisha maendeleo.
Amesema katika mjadala huo wa hadhara kuhusu maendeleo ya kilimo kutoka wakati wa uhuru hadi sasa katika jengo la mikutano la ESRF mjini hapa alisema kwamba tafiti nyingi zimekuwa zikishutumu wakulima kwa kuwa na muono mdogo na kubisha mabadiliko yanayohitaji kuongeza uzalishaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Aidha alisema kwamba kumekuwepo na tafiti zinazoonesha kwamba kilimo kimekwama katika uasili wake na kuhitajika tafiti za kuona namna bora ya kukikwamua.  Hata hivyo alisema profesa huyo, kumekuwepo na mabadiliko ya maana katika uchumi wa vijijini, hasa kwa kuangalia uhalisia wa uchumi kwa kuzingatia fursa za kiuchumi na masoko katika maisha ya wanakijiji.
Alisema kutokana na mabadiliko hayo ni dhahiri kusema kwamba wakulima hawabadiliki ni kushindwa kwa wataalamu ambao ndio walibuni na kupanga mipango ambayo haikuweza kuwanufaisha wakulima.
Profesa Brian Van Arkadie ambaye pia alishawahi kuwa Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam na miongoni mwa watafiti ESRF anasema kuna hatua mbalimbali zilizofikiwa na wakulima wa Tanzania tangu uhuru na kwamba kuna uhusiano kati ya kilimo na maendeleo yaliyopo sasa.
Alisema katika mkutano huo wa hadhara ulilenga kuchambua masuala muhimu yanayojitokeza katika kilimo cha Tanzania na kuona namna bora ya kukabiliana na changamoto hizo kwa maendeleo ya taifa, kuwa kuanzia miaka ya 1970 mazao kwa ajili ya masoko ya nje yaliporomoka sana na kusababisha taifa kutafuta njia nyingine ya kurekebisha hali hiyo ikiwamo kuanzishwa kwa mradi wa kubadili kilimo wa SAGCOT.
Ingawa mazao hayo ya kilimo yameonakana kuporomoka kutoka miaka hiyo, kumekuwepo na ongezeko kubwa la pengo la kipato kati ya watu wa mijini na vijijini huku ukuaji wa vijijini ukikumbwa na  udumavu. Pamoja na ukweli huo amesema profesa huyo, kuna mabadiliko ya kutosha katika maeneo ya vijijini na katika kilimo kwamba kusema hakuna maendeleo si kitu sahihi.
Alisema zipo sababu za kupungua kwa uzalishaji wa mazao makuu kama kahawa, tumbaku, mkonge na  hilo linatokana na serikali kuingilia kati mfumo wa masoko ambao haukuwa unaswihi. Profesa huyo alisema hata hivyo, kwa miaka 50 kilimo cha Tanzania kimefanikiwa kulisha taifa kwa kuwezesha watu wa mijini na vijijini kupata vyakula hasa vile vya msingi ingawa wakati mwingine ukame ulileta usumbufu.
Huku Tanzania ikiwa na ongezeko la watu kutoka milioni 12.3 kwa mwaka 1967 hadi milioni 44.9 kwa mwaka 2012 ni dhahiri ukuaji wa kilimo umesaidia kuiweka nchi katika hali bora zaidi ya upatikanaji wa chakula ingawa ifikapo mwaka 2030 watu wa mijini watakuwa wameongezeka kwa asilimia 37 na kuweka shinikizo ambalo kwa namna nyingine linaweza kuwa na maana kwa kuwa mazao ya chakula yatakuwa ndiyo ya biashara na hivyo kuacha kutegemea yale ya asili kama kahawa na tumbaku.
Katika utafiti mwaka 2007, imeonekana kwamba  nusu ya mapato ya watu wa Dar es salaam yamekuwa yakitumika kwa ajili ya kununua chakula na kufanya kiasi kikubwa cha kazi za kilimo katika mazao ya chakula kuwa biashara nzuri kwa wakulima.Katika mada yake profesa huyo alisititiza kwamba hakuna shaka  maendeleo nchini katika kilimo yapo lakini tafiti nyingi zimeshindwa kuelekeza kisahihi maendeleo hayo na ukweli wa kutoneemeka kwa wakulima.
Akijadili mada hiyo ya Prof. Brian Van Arkadie, Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF Prof Samuel Wangwe ameshauri serikali kutonakili mikakati na sera za nchi zilizoendelea wakati wa utekelezaji wa mikakati ya kugeuza nchi kuwa taifa la uchumi wa kati linalotegemea viwanda.
Alisema hayo katika mhadhara kuhusu kilimo nchini kwamba si sawa kunakili sera na mikakati ya nchi zilizoendelea kama Uingereza, Asia ama Marekani katika kutekeleza sera ya viwanda bali ibuni yenyewe kwa kuzingatia hali iliyopo.
Mhadhiri mwandamizi kitengo cha kilimo uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Aloyce Hepelwa akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van wakati wa mhadhara mkubwa ulioshirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Akizungumza  wakati akijadili mada iliyowasilishwa na Prof Brian Van Arkadie kutoka Uingereza kuhusu mazao ya chakula kama ndio mazao ya biashara katika mikakati ya muda mrefu ya kubadili kilimo cha Tanzania na athari za kisera, Prof Samuel Wangwe alisema kila nchi ina njia yake ya kufikia ustawi na neema ya viwanda na hivyo Tanzania lazima ifuate njia yake na sio kunakili.
“Hatuwezi kupita njia ambayo nchi kama Uingereza, Japan, au nchi za Ulaya zimepita wakati wakikua kiviwanda, lakini tuwe na njia yetu katika kuelekea uchumi wa viwanda . Kama hatutakuwa makini hatutafanikiwa,” alisema.
Prof Wangwe pia alisema kwamba mapinduzi ya Kilimo lazima yapewe kipaumbele kama taifa linataka kuwa na uchumi wa viwanda. Akikaribisha  wadau kushiriki katika mhadhara huo Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kwamba  mhadhara huo ulikuwa ni njia muafaka ya kubadilisha maarifa ili kuboresha kilimo cha Tanzania kwa kukipatia kilimo hicho mkakati wa muda mrefu wa kubadilika.
Alisema katika kuimarisha kilimo hicho ni vyema masuala yanayogusa mazao ya chakula na yale ya kupeleka nje na sera  kuangaliwa kwani masuala hayo yana athari za muda mrefu katika ukuaji wa kilimo.
Katika hadhira hiyo aliwataka washiriki kuangalia kwa makini historia ya kilimo nchini, sera na kuona athari za muda mrefu na fupi za sera zilizopo na kama kweli wataalamu wametekeleza wajibu wao katika kutafuta suluhu ya wakulima au kuendelea kudai kwamba wakulima hawako tayari kubadilika.
Dk. Kida alisema kwa kuangalia historia ya kilimo Tanzania wataalamu hao watakuwa na nafasi kubwa ya kuchangia katika kuendeleza kilimo ambacho ni msingi mkubwa wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kwani wapo asilimia 80 wakitegemea kilimo na taifa ambalo linataka kwenda katika uchumi wa viwanda ambavyo mali ghafi zinategemewa kutoka katika sekta ya kilimo.
Aidha alimshukuru Prof. Brain Van Arkadie ambaye ndiye alikuwa msemaji mkuu kwa utafiti alioufanya ambao aliuwasilisha mbele ya mkutano wa wasomi mbalimbali.
Prof. Van Arkadie ambaye ni veteran ambaye alishawahi kushiriki katika mpango wa miaka mitano wa kwanza wa maendeleo mwaka 1963. Na kufanyakazi katika maeneo mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki na Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: NAFASI YA KILIMO NA SERA ZAKE KATIKA KUFANIKISHA TANZANIA YA VIWANDA
NAFASI YA KILIMO NA SERA ZAKE KATIKA KUFANIKISHA TANZANIA YA VIWANDA
https://1.bp.blogspot.com/-V6tuOfIgwzE/WZ_T2EKA9MI/AAAAAAAAd88/rPsE9dBijEsgB_P_wBheXE83V6TT3WvlgCLcBGAs/s1600/xtulime-750x375.jpg.pagespeed.ic.w6UgsrnDuj.webp
https://1.bp.blogspot.com/-V6tuOfIgwzE/WZ_T2EKA9MI/AAAAAAAAd88/rPsE9dBijEsgB_P_wBheXE83V6TT3WvlgCLcBGAs/s72-c/xtulime-750x375.jpg.pagespeed.ic.w6UgsrnDuj.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/nafasi-ya-kilimo-na-sera-zake-katika.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/nafasi-ya-kilimo-na-sera-zake-katika.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy