NAY WA MITEGO ADAIWA KUFUMANIWA

Nay wa Mitego.
DAR ES SALAAM: MKALI wa Hip Hop Bongo anayesumbua na Wimbo wa Acheze, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amedaiwa kukwaa skendo ya kufumaniwa na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina moja la Tina.
Tukio lililokusanya ‘nzi’ wa kutosha, linadaiwa kutokea hivi karibuni nyumbani kwa msanii huyo, Kimara- Mwisho jijini Dar mida ya saa moja usiku ambapo Nay anadaiwa kuwa, aliingia mchana na gari yake akiwa na mrembo mwingine kabla Tina hajafika ‘kuliamsha dude.’

Chanzo makini kilichoshuhudia mtiti huo mwanzo mwisho, kililipigia simu Amani na kuanika tukio lilivyokuwa kama sinema ya Kihindi:
“Iko hivi, yaani nilitafuta namba zenu wakati tukio linatokea mkawa hampokei, sasa na mimi simu yangu haikuwa na uwezo wa krekodi, ningewapa picha.
“Yaani nilishuhudia mwanzo mwisho kwa sababu mimi naishi maeneo haya na Nay ni jirani yetu. Awali nilimuona Nay akiingia ndani na mrembo mmoja simjui jina lake. Wakaingia ndani. Baada kama ya saa tatu, alikuja mrembo mwingine na Bajaj.

“Sasa huyu aliyekuja na Bajaj alipofika getini, akagonga ndipo akatoka yule mrembo aliyekuja na Nay, ghafla nashangaa wanaanza kurushiana maneno. Yule aliyekuja na Bajaj akawa anamzodoa yule aliyemkuta ndani na kumuambia amefuata nini kwa bwana’ke,” kilieleza chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga ubuyu zaidi, chanzo hicho kilisema mara baada ya kurushiana maneno Nay alitoka na kuwaamulia huku akimuingiza ndani yule binti aliyekuwa naye na kumsihi yule dada aliyekuja kufumania aondoke kabla hajamuitia polisi.
“Nay alikuwa mkali kweli akamuambia yule binti aondoke haraka sana kwani hana mpango naye asije akamuitia polisi, yule dada akawa mpole akaondoka zake,” kilisema chanzo hicho.

Mara baada ya Amani kupewa ubuyu huo ambao tayari ulikuwa umeshatokea, lilimtafuta Nay na kumsomea mashtaka yake yote kuhusu tukio hilo na kumbana kwa kumuambia Amani lina ushahidi wote ndipo akafunguka:
“Hii ishu si kwamba ni fumanizi, huyo Tina aliwahi tu kuwa mpenzi wangu zamani sana, sasa nikashangaa amekuja kufanya fujo home na ndio maana umeona amekuwa mpole baada ya mimi kutokea. Sina mpango naye, ana maisha yake na mimi nina maisha yangu.
“Kwanza hata huyu binti wa watu aliyemletea fujo si mpenzi wangu. Ni msanii ambaye tunafanya naye kazi, bado hajatoka kivile.”
STORI: WAANDISHI WETU, DAR
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post