NAY WA MITEGO: MOND, KIBA, DIMPOZ PIGANENI ATAKAYE KUFA TUTAZIKA

Wakati vita baridi ikiendelea kuunguruma huko mitandaoni kati ya wanamuziki DiamondAlly Kiba na Ommy Dimpoz, rapa Nay wa Mitego ameibuka na kutoa neno lake la kukemea kuwahusisha wazazi katika mabifu yao.

Licha ya Nay kuwahi kuimba kwenye ngoma yake mstari unaosema, “nampenda demu wangu kuliko mama yangu”, lakini ameonekana kuguswa na kuchukizwa na kitendo cha Dimpoz, kumhusisha mama wa Diamond katika ugomvi wao.
nay wa mitego
“Gombaneni, roganeni mpaka muuane, napenda kusikia changamoto kwenye gemu, ila tusiwaingize wazazi wetu tafadhali, tukananeni matusi yote wenyewe kwa wenyewe ikibidi piganeni kabisa atakaye kufa tutazika na itakuwa historia kama Big na Pac.
nay wa mitego
“Ila kuwaingiza wazazi ni ujinga, sipo upande wowote si kwa Kiba, Dimpoz wala Diamond, endeleeni na vita yenu kama wanawake mmechukuliana mabwana, ila suala la wazazi mnavuka mipaka,” aliandika Nay wa Mitego katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram.
NA ISRI MOHAMED/GPL
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post