NEYMAR AMESEPA BARCELONA, SASA KUJIUNGA RASMI PSG

IKIWA takribani miezi miwili tangu tetesi za kuanza kusambaa kuhusu mvutano wa mkali wa Brazil anayekipiga FC Barcelona ya Hispania, Neymar Jr kudaiwa kushinikiza kuhama klabuni hapo ili ajiunge na Paris Saint Germain ya Ufaransa (PSG).
Mapema leo Jumatano, Agosti 2, 2017 Klabu ya Barcelona wamethibitisha kumpa ruhusa Neymar kutofanya mazoezi na timu yao ili kuelekea kukamilisha usajili wake wa kujiunga na PSG. Hiyo ya Barcelona haijaweka wazi sababu za moja kwa moja za ruhusa hiyo.
Kufuatia ruhusa hiyo vyombo vingi vya habari Ulaya vimeripoti kuwa Neymar anaelekea kuanza safari yake ya maisha mapya PSG ambao wameripotiwa kutenga pound Milioni 199 kwa ajili ya kuvunja mkataba wa staa huyo wa zamani wa Santos kiasi kilichopo katika mkataba wake na Barcelona (kuununua mkataba huo).
Endapo uhamisho huo ukikamilika, Neymar ndiye atakuwa mchezaji anayelipwa mkwanja mrefu zaidi duniani na ghali zaidi kuwahi kuuzwa katika historia ya soka.
Kwa kiasi cha pound milioni 199 anachouzwa Neymar ni zaidi ya Tsh Bilioni 580 kiasi ambacho hajawahi kuuzwa wala kununuliwa mchezaji yeyote katika historia ya soka.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post