ORODHA YA MIKOA KUMI INAYOONGOZA KWA KIWANGO KIKUBWA CHA TALAKA

Ni matarajio ya wanandoa wenyewe pamoja pamoja na watu wa karibu kutaka kuona kwamba ndoa inayofungwa na wawili hao idumu ikiwa imejaa upendo, amani na mafanikio yote ambayo binadamu tunaweza kuyafikiria.
Labda kutokana na shauku ya kutaka kufanikisha sherehe hii ya kuoana ndio sababu wengine hujikuta wakificha baadhi ya tabia zao halisi kwa wapenzi wao (kabla ya kuoana) ili lengo lao la kuujulisha umma kwamba na yeye ameoa au kuolewa. Baada ya kuingia kwenye ndoa, makucha huanza kuchomolewa taratibu na kusababisha kero kwa mwenzake.
Hili husababisha migogoro kwenye ndoa – na mara nyingine migogoro hiyo huwa mikubwa kiasi cha kusababisha ndoa hiyo iliyofungwa kwa shangwe kufikia tamati. Kutegemea kiwango cha uvumilivu wa mwenza au kiwango cha maudhi yenyewe, ndoa hii yaweza kuvunjika mwezi mmoja tu au miwili baada ya harusi au kudumu kwa miaka kadhaa kabla ya kufikia mwisho.
Utafiti wa mwaka 2014/15 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) unaonesha kuwa kiwango cha talaka kimeongezeka kutoka asilimia 1.1 mwaka 2008/09 mpaka asilimia 2.1 mwaka 2014/15.
Takimu hizi zinasema kuwa, mikoa kumi yenye kiwango kikubwa cha talaka ni kama ifuatavyo:
Mkoa wa Kusini Unguja unaongoza kwa kuwa na asilimia 5.3 cha talaka nchini ukifuatiwa na Mkoa wa Mtwara (wenye asilimia 4.8), Mkoa wa Mjini Magharibi (wenye asilimia 4.6), Mkoa wa Lindi (wenye asilimia 4.6), Mkoa wa Kaskazini Unguja (wenya asilimia 4.2) na Mkoa wa Pwani (wenye asilimia 4.1)
Mikoa hii sita ndiyo inayoongoza kwakuwa ina kiwango kikubwa zaidi cha asilimia nne ambacho kipo juu ya wastani wa kitaifa wa asilimia tatu kwa mujibu wa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Mikoa mingine yenye kiwango kinachofata ni Kusini Pemba (wenye asilimia 3.7), Mkoa wa Kaskazini Pemba wenye asilimia 3.5), Mkoa Morogoro (wenye asilimia 3.5) na Mkoa wa Dar es salaam (wenye asilimia 3.3)
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), si wanandoa wote wanaotalakiana mahakamani wanapeleka matamko ya talaka hizo kwa wakala kwao ndio sababu kumbukumbu zilizopo RITA zinaonesha kuwa kiwango cha talaka nchini ni kidogo huku mwenendo halisi wa mtaani ukionesha kinyume chake.
Mbali na talaka, kuna wanandoa wanne kwa kila 100 ambao wametengana, jambo linaloashiria kuwa huenda nao wakatalikiana siku zijazo iwapo hawatapata suluhu ya kudumu ya tofauti zao.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post