PANYA WAMFUKUZA RAIS WA NIGERIA OFISI

Rais Buhari wa Nigeria atalazimika kufanya kazi akiwa nyumbani kwake kwa muda wa miezi mitatu baada ya kurejea nchini humo akitokea Uingereza alipokuwa akipatiwa matababu baada ya mapanya kuharibu samani za ofisi yake.
Msemaji wa Rais wa Nigeria ameiambia BBC kuwa, Ofisi ya Rais Buhari inakarabatiwa baada ya panya kuharibu samani zake pamoja na viyoyozi.
Aliongeza kuwa, Buhari hawezi kufanya kazi katika ofisi yake kutokana na hali yake ya sasa ambapo akifanyia kazi akiwa nyumbani hakutaathiri maendeleo yake kiafya.
Rais Buhari alirejea Nigeria Jumamosi iliyopita baada ya kukaa nchini Uingereza kwa muda wa siku 103 akipatiwa matibabu lakini ugonjwa anaougua haujawekwa wazi.
Tangu muda huo alipowasili Nigeria amekosolewa katika mitandao ya kijamii kufuatia kushindwa kuwaeleza wananchi wake anasumbuliwa na tatizo gani.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post