PICHA 13: NEYMAR JR BAADA YA KUTUA RASMI PSG AKITOKEA BARCELONA

Nyota wa soka wa Brazil, Neymar Jr ametambulishwa rasmi na klabu yake mpya ya Paris Saint-Germain (PSG) ya nchini Ufarasa baada ya kukamilisha usajili kutoka Barcelona kwa ada ya uhamisho ya Tsh 579 bilioni ambayo imevunja rekodi ya dunia.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Neymar alisema kwa muda mrefu alikuwa hajui hatma yake na kwamba, wachezaji wengi wa Brazil walikuwa wakimshawishi ajiunga na PSG.
Aidha, Neymar ambaye hakueleza sababu za kuamua kuikimbia Barcelona, amesema kwamba hajajiunga na PSG ili awe mchezaji mkubwa klabuni hapo.
Akieleza masikitiko yake, Neymar alisema kwamba bado anaiheshimu klabu ya Barcelona lakini amesikitishwa na ukosoaji uliofanywa na mashabiki huku baadhi yao wakienda mbali na kuchoma jezi zake.
Kutokana na uhamisho huo wa ghali zaidi duniani,  Neymar atalipwa mshahra baada ya makato Tsh 1.6 bilioni kwa wiki ambapo kwa mwezi atalipwa Tsh 6.4 bilioni akiitumikia PSG.
Hapa chini ni picha 13 zNeymar leo akitambulishwa;

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post