PICHA: DIAMOND NA ZARI & HARMONIZE NA MPENZI WAKE WALIVYOKULA BATA JANA NAIROBI

Kwa muda wa siku kadhaa mwanamuziki anayetamba na ngoma ya Eneka, Diamond Platnumz amekuwa nchini Kenya ambapo yupo mapumziko na mzazi mwenzake Zari The Boss Lady katika Mji wa Mombasa.
Lakini jana wakimalizia wikiendi yao waliamua kubadilisha viwanja vya kuserebuka ambapo walikuwa Club B jijini Nairobi ambapo waliungana pia na Harmonize na mpenzi wake. Uwepo wao ulisababisha club hiyo kujaa mashabiki wengi ambao hawakutaka kukosa kuwaona mastaa hao kutoka Tanzania.
Diamond alitumbuiza nyimbo kadhaa na kisha Zari alipata nafasi ya kuzungumza na mashabiki zake kabla ya Harmonize na yeye kulitawala jukwaa kwa kutoa burudani.
Licha ya kuwa mpenzi wa Harmonize hakuonekana kuchangamka kama ilivyokuwa kwa Zari, lakini furaha yake ilionyesha wazi kuwa alifurahia uwepo wake eneo hilo.
Hapa chini ni picha za tkio hilo jana;

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post