PICHA ZA NGONO KWENYE SIMU ZAMPELEKA MWANAFUNZI JELA MIAKA 20

MWANAFUNZI wa Chuo cha Utumishi wa Umma  mjini Tabora, Marick Mbega amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 jela baada ya kutiwa hatiani kudhalilisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Isike.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora, Emanuel Ngigwana baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka wakiwamo wanafunzi wiwili waliodhalilishwa.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Upendo Malulu alidai mahakama Marick alitenda makosa hayo AprilI 4, mwaka huu kinyume na kifungu namba 138 A cha kanuni za adhabu  sura ya 16 ya 2002.
Wakili huyo aliendelea kusema mahakamani hapo kwamba mtuhumiwa huyo aliwaonyesha wanafunzi wa shule hiyo picha za kongo kwa kutumia simu yake ya mkononi jambo ambalo alijua ni kinyume na sheria pamoja na maadili ya kitanzania.
Mtuhumiwa huyo inaelezwa kuwa hakuishia katika kuwaonyesha wanafunzi hao picha hizo bali aliwashawishi wanafunzi hao wamshike sehemu za siri huku na yeye akiendelea kuwachezea.
Ndani ya simu ya mkononi ya Mbega, Wakili Malulu aliiambia mahakama kuwa walikuta picha 197 za ngono na video 40 za wanyama, watoto na watu wazima baada ya kuifanyia upekuzi.
Hakimu alisema kitendo alichokifanya Mbega kinachukuliwa kama udhalilishaji kwa sababu watoto hawana maamuzi hivyo hawawezi kuchukuliwa kama walikubali kutazama picha hizo pamoja na kuchezewa sehemu zao za siri. Watoto wanatakiwa kukukuwa salama kamaadili, kiakili hivyo kuwaonyesha picha za ngono na kuwachezea sehemu za siri ni kuwadhalilisha.
Upande wa mashtaka uliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kudhalilisha watoto katika jamii.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post