RAIS DKT MAGUFULI AMPONGEZA UHURU KENYATTA KWA USHINDI

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza Rais Mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne Agosti 8 mwaka huu.
Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) alimtangaza Rais Uhuru Kenyatta mshindi jana Agosti 11 majira ya saa nne usiku baada ya matokeo hayo ya uchaguzi uliogubikwa na ushindani mkubwa kusubiriwa kwa hamu na watu mbalimbali.
Katika salamu za pongezi alizotoa Rais Dkt Magufuli, amemtakia mafanikio mema Rais Kenyatta katika kipindi kingine cha uongozi wake.
Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema.

Mbali na Rais Magufuli, viongozi wengine waliompongeza Rais Kenyatta kwa ushindi huo ni pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Nkurunziza wa Burundi, Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Congratulations my brother @UKenyatta for a successful election and the trust Kenyans have placed in you!


On behalf of all Burundians, I congratulate President elect @UKenyatta and the people of Kenya. Looking forward to strengthen our relations.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post