RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA FERI DAR NA KUTOA MAAGIZO KWA RC MAKONDA

SHARE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Feri na kisha kuvuka bahari kwa kutumia kivuko cha MV Kigamboni ambako amekutana na wananchi wa Kigamboni, ametembelea Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere na ametembelea Daraja la Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukata tiketi yake Mhe. Rais Magufuli amepata wasaa wa kuzungumza na wananchi aliosafiri nao katika kivuko cha MV Kigamboni na baadaye kuzungumza na wananchi wa Kigamboni ambapo ameulizwa na kujibu mambo mbalimbali.
Kuhusu ubovu wa barabara Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali imechukua hatua ya kukabiliana  na tatizo hilo kwa kuanzisha Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) ambayo itafanya kazi ya kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami.
Kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme amesema Serikali inatekeleza miradi mbalimbali itayoongeza kiwango cha umeme katika gridi ya taifa pamoja na kurekebisha miundombinu yake na amewaomba kuwa na subira wakati juhudi hizo zinaendelea.
Akiwa katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere Mhe. Rais Magufuli amekutana na vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka vyuo na vyuo vikuu vya Mkoa wa Dar es Salaam waliopiga kambi katika chuo hicho, ambao wamempongeza kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya kuiongoza Serikali ya Awamu ya Tano ambayo kwa muda mfupi imeonesha uongozi unaoacha alama.
Vijana hao wamemhakikishia kuwa wanamuunga mkono na wamemuahidi kuwa wapo tayari kuitumikia nchi kwa jukumu lolote watakalopewa na kwamba daima watatanguliza maslahi ya nchi.
Akizungumza na vijana hao Mhe. Rais Magufuli amewapongeza kwa moyo wa uzalendo waliouonesha, na amewataka kuwa nguzo imara ya mabadiliko ya kweli nchini ili juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kurekebisha mambo yaliyosababisha kukiuka misingi ya Waasisi wa Taifa zizae matunda.
Mhe. Rais Magufuli ameeleza baadhi ya juhudi hizo kuwa ni kukabiliana na rushwa inayodhohofisha uchumi na huduma za kijamii, kudhibiti mianya ya matumizi mabaya na upotevu wa fedha na mali za umma, kuondoa watumishi hewa na wenye vyeti vya kughushi, kuongeza bajeti ya maendeleo katika bajeti ya Serikali, kuongeza uzalishaji wa umeme, kujenga viwanda, kujenga reli, kununua ndege za Serikali, kuongeza ukusanyaji wa kodi na kuchukua hatua kali dhidi ya wahujumu uchumi.
“Nataka niwahakikishie vijana wote kuwa nawapenda sana, hata mimi nilikuwa Umoja wa Vijana, yote yaliyotokea kinyume na misingi ya chama hiki na misingi ya waasisi wetu wakiongozwa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere nimeamua kuyanyoosha na yatanyooka, na nyinyi simameni imara, kitumikieni chama na msitumikie watu au vikundi vya watu, mkifanya hivyo kila kitu kitakwenda vizuri kabisa” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli amewataka vijana hao kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa chama utakaofanyika baadaye mwaka huu, na amebainisha kuwa wasiwe na hofu ya kuwepo kwa rushwa kwa kuwa wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa hawatapitishwa kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama.
Pia amewaambia viongozi wa Secretarieti ya CCM aliowakuta wakizungumza na vijana hao kuwa anazo taarifa zote juu ya watu waliojimilikisha mali za chama na amesema anasubiri wakati ukifika achukue hatua zinazostahili.
Baada ya kuzungumza na vijana hao Mhe. Rais Magufuli ametembelea Daraja la Nyerere na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo, ambapo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda kufanyia kazi ombi la wananchi kujengewa kituo cha Daladala.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
25 Agosti, 2017

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA FERI DAR NA KUTOA MAAGIZO KWA RC MAKONDA
RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA FERI DAR NA KUTOA MAAGIZO KWA RC MAKONDA
https://4.bp.blogspot.com/-AJ3VUV7OSnk/WaA3lrN652I/AAAAAAAAd-U/3hF2_hT-ylc_B0KTh7GnxnZGpL20ZRbhQCLcBGAs/s1600/Magufuli-na-Makonda.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-AJ3VUV7OSnk/WaA3lrN652I/AAAAAAAAd-U/3hF2_hT-ylc_B0KTh7GnxnZGpL20ZRbhQCLcBGAs/s72-c/Magufuli-na-Makonda.jpg
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/rais-magufuli-afanya-ziara-ya.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/rais-magufuli-afanya-ziara-ya.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy