RAIS MAGUFULI AHANI MSIBA WA MWALIMU WAKE WA CHUO KIKUU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Agosti, 2017 amewapa mkono wa pole familia ya Dkt. Steven Juma Mdachi aliyefariki dunia jana tarehe 01 Agosti, 2017 katika Hospitali ya Tumaini Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Dkt. Steven Juma Mdachi alikuwa Mhadhari wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Uhandisi, Idara ya Kemia.
Akiwa nyumbani kwa Marehemu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Rais Magufuli ametia saini kitabu cha maombolezo na kuwapa mkono wa faraja Mjane wa Marehemu Mama Mary Mdachi, watoto wa Marehemu, wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na ndugu jamaa na marafiki.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post