RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ZAMANI WA JAPAN

SHARE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Agosti, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Mbung...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Agosti, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Mbunge na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Mhe. Ichiro Aisawa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika Mazungumzo hayo Mhe. Ichiro Aisawa amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi mzuri, kupambana na rushwa na msukumo mkubwa anaoutoa katika maendeleo, juhudi ambazo zinasaidia kuimarisha uchumi na kuboresha huduma za kijamii.
Mhe. Ichiro Aisawa ambaye ametembelea baadhi ya miradi inayojengwa hapa nchini na kampuni za Japan ukiwemo mradi wa ujenzi wa barabara za juu (Flyover) wa TAZARA na Mradi wa kuzalishaji umeme kwa gesi wa Kinyerezi amemhakikishia Mhe. Rais Magufuli kuwa kampuni hizo zitafanya kazi nzuri na zitakamilisha kazi kama ilivyopangwa.
Pia Mhe. Ichiro Aisawa amesema baada ya kuona changamoto ya foleni katika Jiji la Dar es Salaam amebaini kuwa nchi yake bado inahitaji kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam na ameahidi kufikisha ujumbe huo kwa Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Shinzo Abe.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Ichiro Aisawa kwa kuja Tanzania na amemhakikishia kuwa Tanzania inatambua mchango mkubwa ambao Japan inautoa katika maendeleo, na itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Japan katika masuala mbalimbali.
Mhe. Rais Magufuli ameishukuru Japan kwa kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi Jijini Dar es Salaam ikiwemo upanuzi wa barabara ya Mwenge – Morocco utakaoiwezesha barabara hiyo kuwa na zaidi ya njia nane, ujenzi wa barabara ya TAZARA, ujenzi wa Daraja la Gerezani njia nne, na barabara ya Bendera tatu hadi Kamata.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemuomba Mhe. Ichiro Aisawa ambaye ni mwakilishi wa wabunge wa Japan wanaoshughulikia masuala ya Afrika kuwahamasisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Japan kuja kuwekeza hapa nchini na ameahidi kuwa Serikali itahakikisha uwekezaji wao unalindwa kama itakavyofanya kwa kampuni ya kutengeneza rangi ya Kansai Plascon ambayo awali ilijulikana kama Sadolin, na kampuni inayozalisha Betri za Panasonic hapa nchini, ili uwekezaji huo ulete manufaa hapa nchini.
“Naomba unifikishie ujumbe kwa Waziri Mkuu Shinzo Abe kuwa Tanzania inamshukuru kwa ushirikiano huu mkubwa, tunamkaribisha sana Tanzania na kwa kuwa Serikali yetu imehamia Dodoma tutafurahi sana kama Japan itaweka alamu ya urafiki wetu kwa kutujengea barabara za Dodoma mjini, iwe ni flyover au kilometa 20 za barabara, sawa tu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
15 Agosti, 2017

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ZAMANI WA JAPAN
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ZAMANI WA JAPAN
https://1.bp.blogspot.com/-m_UYO-58UBQ/WZPwcdmwAfI/AAAAAAAAdic/_r8GqQ1dhPsfJjJ-gsmaKGwlS6zj6uMVwCLcBGAs/s1600/xunnamed-11-1-1-673x375.jpg.pagespeed.ic.-lEROXQSFa.webp
https://1.bp.blogspot.com/-m_UYO-58UBQ/WZPwcdmwAfI/AAAAAAAAdic/_r8GqQ1dhPsfJjJ-gsmaKGwlS6zj6uMVwCLcBGAs/s72-c/xunnamed-11-1-1-673x375.jpg.pagespeed.ic.-lEROXQSFa.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/rais-magufuli-akutana-na-waziri-wa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/rais-magufuli-akutana-na-waziri-wa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy