RAIS MAGUFULI AWAPATANISHA RUGE NA MAKONDA

Leo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewapatanisha Mkurugenzi wa Kituo cha Utangazaji cha Clouds Media Group, Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Hayo yametokea leo mkoani Tanga, katika sherehe za kuweka jiwe la msingi la mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Tanga-Tanzania.
Rais Magufuli aliwataka wawili hao wafanye kazi kwa bidii kwa lengo la kuiinua Tanzania ili ifike uchumi wa kati. Vilevile alimpongeza Ruge Mutahaba kwa utunzi mzuri wa wimbo wa Tanzania wenye dhumuni la kudumisha amani nchini.
“Nataka mambo yenyu ninyi wawili yaishe, nataka mfanye kazi kwa ajili ya Tanzania. Nampongeza Ruge kwa nyimbo nzuri na Mungu awabariki sana” alisema Rais Magufuli.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post