RIPOTI YA MKEMIA WA SERIKALI KUHUSU SAMPULI YA MKOJO WA AGNESS MASOGANGE

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imepokea taarifa ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilioonesha kwamba sampuli ya mkojo wa Agnes “Masogange” Gerald una chembechembe za dawa za kulevya.
Aidha, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametupilia mbali pingamizi la kutopokea ushahidi huo la upande wa utetezi kwa madai kuwa, fomu zilizopelekwa kwa mkemia hazikufata sheria.
Amesema mahakamani hapo kuwa, shahidi wa kwanza ambaye ni Elia Mulima anahaki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti mahakamani.
Ameongeza polisi walipeleka maombi kwa mkemia wa serikali na kwamba ni wazi mshitakiwa alienda kwa mkemia na askari wawili na kumpatia kontena kwa ajili ya kuweka sampuli ya mkojo. Kesi imeahirishwa kwa muda.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post