ROMA KWA UJIO WAKO HUU, HATA VIZIWI WATASIKIA!

Mwanaharakati aliyeiteka gemu ya muziki wa Hip Hop Bongo, kutokana na tungo zake, Roma Mkatoliki, baada ya kupotea kwa muda mrefu kwenye gemu hatimaye amerudi upya kwa kishindo na ngoma inayoitwa Zimbabwe.
Katika ngoma hiyo Roma ameongelea zaidi kuhusu tukio la kutekwa kwake, jinsi familia yake ilivyoteseka kumtafuta, pamoja na kuwashukuru wote waliopaza sauti zao katika jitihada za kumtafuta.
“Wengi mlijiuliza walioniteka ni maaskari mkanitafuta vituo vyote Central hadi Staki Shari, wakasema hawajui nilipo mama alienda hadi mochwari dah!
“Mwanangu alimuuliza mama baba lini atarudi? Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sina budi, kipi bora nife mseme nimekufa kiharakati, siogopi kufa ila nawaachaje wanaobaki?
“Kutekana tekana ni uhuni wa kishamba na waliosadiki Roma ataonekana kabla ya Jumapili, God blessimetimia injili niliyoitabiri”
Hiyo ni baadhi ya mistari inayopatikana kwenye wimbo huo wa Zimbabwe.
Tukio la Roma, msanii mwenzake Moni, na prodyuza wake Bin Laden kutekwa na watu wasiojulikana lilitokea miezi minne nyuma, ambapo tarehe 8 Aprili mwaka huu walirejea wakiwa na majeraha mwilini, na mpaka sasa kesi yao bado ipo katika vyombo vya sheria.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post