SAIDA KAROLI AIBIWA, ATISHIWA KIFO

Saida Karoli.
DAR ES SALAAM: Mwanamama anayefanya vizuri kupitia Muziki wa Asili Bongo, Saida Karoli siku chache zilizopita alivamiwa na watu wasiojulikana na kumuibia yeye na wacheza shoo wake vitu mbalimbali vya thamani vikiwemo simu za mikononi, fedha kabla ya kutishiwa kuuawa na mtu mwingine asiyefahamika.

Akizungumza na Ijumaa jana, mwimbaji huyo ambaye wimbo wake wa Olugambo unafanya vizuri kwenye media mbalimbali Bongo hivi sasa, alisema tukio la kuibiwa limetokea hivi karibuni mkoani Geita kwenye Ukumbi wa Ambasador na baada ya tukio hilo mtu asiyejulikana alimpigia simu na kumwambia kuwa ametumwa kumuua.

“Nilishituka sana kusikia kuwa huyo mtu alitumwa kuniua. Nikamuuliza kama ametumwa kuniua, alikuwa ananiambia ili iweje, akaniambia kuwa hakuhitaji kufanya jambo kama hilo maana alikuwa ananiona sina hatia.

IJUMAA: Hukumuuliza alitumwa na akina nani?
SAIDA: Nilimuuliza, lakini alichoniamba eti ni kina mama wawili ambao mimi nina ugomvi nao.

IJUMAA: Hao kina mama unawafahamu?
SAIDA: Hapana. Mimi sina ugomvi na mtu yeyote, kwa hiyo nilibaki tu kushangaa na alichokuwa akiniambia.

IJUMAA: Hakuna cha zaidi ambacho mlizungumza naye?
SAIDA: Zaidi ni kwamba eti watu hao walikuwa wanaisaka roho yangu muda tu maana walikwisha leta dawa na kumwaga mlangoni lakini kwa bahati nzuri kwangu hazikuweza kunishika.

IJUMAA: Umeripoti polisi juu ya tukio hilo?
SAIDA: Nipo kwenye ‘prosesi’ hizo.

IJUMAA: Vipi kuhusu matamasha yako ya Kanda ya Ziwa?
SAIDA: Kutokana na hiki kilichotokea, nimeamua kusitisha matamasha hayo, ngoja nifuatilie kwanza juu ya hili suala la maisha yangu halafu baadaye ndiyo nitatoa taarifa kuwa shoo nitafanya lini.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post