SERIKALI KUBOMOA NYUMBA YA MKE WA RAIS MKAPA

SHARE:

Wakati zoezi la ubomoaji na uwekaji alama katika nyumba zinazotakiwa kubomolewa likiendelea jijini Dar es Salaam, nyumba ya Anna Mkapa, M...

Wakati zoezi la ubomoaji na uwekaji alama katika nyumba zinazotakiwa kubomolewa likiendelea jijini Dar es Salaam, nyumba ya Anna Mkapa, Mke wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Benjamin Mkapa imekumbwa na bomoabomoa inayoendelea pembeni mwa Barabara ya Morogoro baada ya kuwekewa alama ya “X”.
Nyumba hiyo ipo kwenye shamba linalomilikiwa na familia ya Mkapa lililopo eneo la Mbezi kwa Msuguri, maarufu kwa jina la Kituo cha Zamani na ubomoaji huo unafanyika ili kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro inayounganisha Dar es Salaam na mikoa mingine.
Ingawa kijana aliyekuwepo hakuwa tayari kutoa maelezo, nyumba hiyo imezungushiwa ukuta na ina lango lililopakwa rangi nyeusi na ina duka ambalo muuzaji amewekwa na msimamizi wa mali hiyo.
Mmoja wa watu waliokutwa katika nyumba hiyo alisema kuwa, kweli nyumba hiyo ni ya Mama Anna lakini hawezi kuzungumza chochote na kwamba awasiliane na mmiliki.
“Ni kweli hapa ndiyo nyumbani kwa mama Anna Mkapa, lakini mimi siwezi kuzungumza chochote kwa sababu si mhusika. Hapa ni kama mwangalizi wa nyumba tu. Naomba mtafute mama (Anna Mkapa) mwenyewe. Nendeni ofisini kwake. Mimi hapa ameniachia tu kama mwangalizi wa nyumba yake, kwa hilo mtanisamehe siwezi kuzungumza,” alisema .
Hata hivyo, mmoja wa wafanyakazi wa ndugu wa mke huyo wa Rais wa zamani ambaye alikuwa akiuza duka lililoko nje ya nyumba hiyo, alisema atafutwe mtu mmoja aliyemtaja kuwa ni “babu mmoja kipofu”.
“Naomba mkamuone babu mmoja kipofu na yeye nyumba yake imewekewa alama ya “X” anaweza kuwa na taarifa juu ya nyumba hii kwani nimekuwa nikimsikia akizungumza,” alisema.
Babu huyo alipotafutwa na kupatikana alijitambulusha kama James Shirinde (80) na alianza kueleza jinsi alivyonunua eneo hilo ambalo kwa sasa linamilikiwa na familia ya Mkapa.
“Nilinunua eneo hilo mwaka 1975 wakati huo nikiwa mfanyakazi wa Shirika la Reli ambalo kwa wakati huo lilijulikana kama TRC na huku kulikuwa ni mashamba tu,” alisema.
“Mwaka 1980, mke wa rais mstaafu alikuja akanunua shamba na akajenga nyumba ambayo mpaka sasa anaishi mdogo wake, Rose Silayo.”
“Haya mawe waliyoyaweka sasa yametukuta baada ya kutungwa sheria mpya ya Hifadhi ya Barabara ya mita 121.5 mwaka 2007 na 2009. Wakati huo mke wa Mkapa naye alikuwa amejenga nyumba yake na mumewe pia alikuwa amenunua shamba huku la ekari tano,” alisema.
Injinia wa TANROADS, Johnson Letechura alipoulizwa kuhusu alama ya bomoa katika nyumba hiyo, alijibu kwamba nyumba yoyote ambayo ipo katika hifadhi ya barabara itabomolewa.
Chanzo: Mwananchi

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: SERIKALI KUBOMOA NYUMBA YA MKE WA RAIS MKAPA
SERIKALI KUBOMOA NYUMBA YA MKE WA RAIS MKAPA
https://1.bp.blogspot.com/-_6O0RKTIrCI/WZLHTgUP_3I/AAAAAAAAdh4/YM77lKf52Qk6cMaKvafH-MDWsCWxeRo8wCLcBGAs/s1600/xMKAPAANNA-592x375.jpg.pagespeed.ic.x_-bQn6DbV.webp
https://1.bp.blogspot.com/-_6O0RKTIrCI/WZLHTgUP_3I/AAAAAAAAdh4/YM77lKf52Qk6cMaKvafH-MDWsCWxeRo8wCLcBGAs/s72-c/xMKAPAANNA-592x375.jpg.pagespeed.ic.x_-bQn6DbV.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/serikali-kubomoa-nyumba-ya-mke-wa-rais.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/serikali-kubomoa-nyumba-ya-mke-wa-rais.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy