SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAONGEZA MAFAO KWA WASTAAFU

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya marekebisho ya malipo ya pensheni kwa wastaafu kutoka shilingi 40,000 hadi kufikia kiwango cha shilingi 90,000 kwa kima cha chini kwa mwezi.
Akizungumza na waandishi wa habari visiwani Zanzibar, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Khalid Salum Mohammed alisema kiwango hicho kipya cha wastaafu kimeanza kulipwa tangu Julai mwaka huu kwa ongezeko la asilimia 125.
Alisema kuwa jumla ya wastaafu 12,182 waliosajiliwa kwa sasa wamepatiwa kiwango hicho ingawa kulikuwa na changamoto katika kupata taarifa zao za utumishi.
“Kabla ya marekebisho haya, kima cha chini cha pensheni kwa wastaafu kilikuwa shilingi 40,000 kwa mwezi. Hiki tulisema kiongezwe kulingana na gharama za maisha,” alisema.
Alisema kiwango hicho kipya kinaleta uwiano kwa kiwango cha chini kinacholipwa na mfuko wa hifadhi ya jamii cha asilimia 30 ya kima cha chini cha mshahara.
Alisema kuwa serikali pia inaendelea kufanya mapitio ya pensheni za wastaafu ambao walikuwa na nyadhifa serikalini na mapitio hayo bado yanaendelea.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post