SERIKALI YAANZA UJENZI WA MAABARA YA NYUKLIA

Serikali imetenga shilingi bilioni 2.3 kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya kisasa ya nyuklia katika Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC). Lengo la maabara hiyo ni kutoa huduma bora za kisasa za masuala ya mionzi kwa nchi za Afrika.
Aidha, vifaa vyenye thamani ya shilingi bilioni 11.5 kwa ajili ya maabara hiyo vilivyotolewa na Umoja wa Ulaya (EU) vimeanza kuwasili nchini na kuhifadhiwa kwenye maabara za tume hiyo.
Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara hiyo jana, Waziri wa Elimu, Sayansi, na teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema shilingi bilioni 2.3 hizo zimetolewa na Serikali na zimetokana na fedha za ndani.
Alisema Serikali imetoa kwanza shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo linalotarajiwa kukamilika Februari mwakani. Kiasi kilichobaki cha shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo kitafuatia ili maabara hiyo ya kisasa iweze kutumiwa na watu mbalimbali nchini na Afrika nzima.
“Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwezesha,” alisema Profesa Ndalichako. “Maendeleo ya nchi yanasongwa hasa katika kuhakikisha tume hii inapata maendeleo na kuchangia fedha katika mfuko huu wa Serikali.”
Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Brigedia Jenerali Fulgence Msafiri, alisema maabara hiyo itatoa huduma mbalimbali za matumizi salama ya mionzi pamoja na kuwa msaada kwa wanafunzi wa vyuo vikuu katika ngazi ya shahada ya Uzamili na uzamivu.
HT @ Nipashe
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post