SERIKALI YAELEZA SABABU YA KUCHELEWA KULETWA KWA NDEGE NYINGINE MPYA

Baada ya ndege mbili aina ya Bombardier Dash 8Q400 kuwasili nchini, serikali iliahidi kununua ndege nyingine kwa ajili ya kuimarisha usafiri wa anga pamoja na kuinua sekta ya utalii nchini ambapo watalii wangeweza kuja nchini moja kwa moja bila kupitia nchi nyingine.
Miongoni mwa ndege mpya ambazo zitanunuliwa na serikali ni Bombardier ambayo serikali ilisema kwa ingewasili nchini Julai 2017 lakini hadi sasa ndege hiyo haijafika.
Akitaka kujua mpango huo umeishia wapi, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe jana alimuuliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa kuwa mpango huo umeishia wapi kwani muda wa ndege hiyo kuwasili nchini tayari umepita.
Waziri @MbarawaM Serikali iliahidi Bungeni kuwa mwezi July mtapokea Ndege nyengine Bombadier. Leo ni August imepinduka. Ndege [z]ipo wapi?

Akijibu swali hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter, waziri mwenye dhamana alisema ni kweli kwamba serikali iliahidi ndege hiyo zingefika Julai, lakini kuna taratibu ambazo hazijakamilika, na zitakapokamilika, ndege hiyo itatua nchini.
Waziri @MbarawaM Serikali iliahidi Bungeni kuwa mwezi July mtapokea Ndege nyengine Bombadier. Leo ni August imepinduka. Ndege [z]ipo wapi?
Mhe. Ni kweli kabisa ahadi ilikuwa July kuna taratibu za mwisho zafanywa kabla ya kuwasili hivyo itawasili tu

Zitto Kabwe alipotaka kujua taratibu hizo ambazo hazijakamilika na kufanya ndege hiyo kuchelewa kwa mwezi mmoja sasa, waziri huyo hakueleza zaidi.
Rais Magufuli amewahi kunukuliwa akisema, Tanzania inapanga kununua ndege aina ya Boeing 787 Dash 8 Dreamliner yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini humo Juni 2018.

Ndege nyingine ambazo Tanzania itazinunua ni ndege moja aina Bombardier Q400 Dash 8 NextGen ambayo ndiyo waziri amesema itawasili muda wowote taratibu zikikamiliwa, ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 na zinazotarajiwa kuwasili nchini kati ya Mei na Juni, 2018.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post