SERIKALI YAITAJA KAMPUNI YA MANJI ITAKAYOIFUTA KWA KUKIUKA SHERIA

SHARE:

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kusudio la kufuta leseni ya Kampuni ya Mycell inayomilikiwa na Quality Group Limited (Q...

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kusudio la kufuta leseni ya Kampuni ya Mycell inayomilikiwa na Quality Group Limited (QGL) ambayo imekuwa ikiongozwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Yussuf Manji.
Kwa mujibu wa sheria, TCRA iliyoanzishwa mwaka 2003 ina jukumu la kusimamia, kutoa na kufuta leseni za mawasiliano kwa kampuni yoyote ambayo imeshindwa kutekeleza majukumu iliyoyabainisha.
“Kampuni ya Mycell imeshindwa kurekebisha ukiukwaji wa masharti ya leseni”, inasomeka taarifa iliyotolewa na kuwekwa kwenye tovuti ya mamlaka hiyo.
Kutokana na upungufu huo, “TCRA inauarifu umma kuhusu kusudio la kufuta leseni za Mycell za kujenga miundombinu kitaifa, kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo, kutoa huduma kupitia mtandao na kutumia masafa ya mawasiliano”.
Kuonyesha juhudi ilizochukua kabla ya uamuzi huo, TCRA imesema Januari 27, 2016 ilitoa amri ya utekelezaji kwa kampuni hiyo kwa kukiuka masharti ya leseni walizopewa na kushindwa kutoa huduma kinyume cha kifungu 21 (a) na (b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielekrtoniki na Posta (Epoca) ya mwaka 2010.
Hata hivyo, Mycell haimo kwenye orodha ya kampuni zilizopewa leseni na TCRA ambazo zimo kwenye tovuti ya mamlaka hiyo.
Mamlaka hiyo imeeleza kwenye taarifa yake ya kusudio la kuifuta Mycell kuwa iliipa kampuni hiyo leseni nne tofauti Novemba 21,2008.
Inafafanua kuwa leseni hizo ni ya kujenga miundombinu kitaifa, kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo, kutoa huduma kupitia mtandao wa mawasiliano na kutumia masafa ya mawasiliano.
Kwenye ujumbe wake alioutoa Oktoba, 2011 wakati Quality Group ikitimiza miaka 35 tangu ianzishwe nchini, mwenyekiti Yusuf Manji alitanabaisha vipaumbele vya utekelezaji walivyonavyo.
“Mycell inatekeleza mpango wa biashara unaoiruhusu kukodisha masafa iliyopewa na TCRA kwa kampuni ya nje yenye uwezo na uzoefu mkubwa. Inatarajia kujenga miundombinu imara itakayofanikisha miradi mbalimbali”, alisema Manji.
Alisema mpango huo unatokana na fursa kemkem zilizopo kwenye sekta ya mawasiliano nchini hasa kwa kuzingatia njia za kawaida za kufikishiana ujumbe ambazo zimekuwa hazikidhi mahitaji yaliyopo kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia hasa ya habari na mawasiliano (Tehama).
“Sekta hii ina fursa nyingi kwa kampuni zenye teknolojia ya kisasa kuwekeza na kukua. QGL inaona kwamba kuna haja ya kuwekeza kwenye miundombinu na kuziruhusu kampuni za mawasiliano kuongeza ufanisi. Gharama za kupiga simu na data zipo juu nchini ikilinganishwa na ilivyo kwa nchi za Asia zinazonufaika na Tehama kwa kiasi kikubwa”, alisema Manji kwenye ujumbe wake wa mwaka 2011.
Mwaka 1997,Manji alianza kuiongoza QGL akihudumu kama ofisa mtendaji mkuu kabla ya baadaye kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kundi hilo, nafasi aliyojiuzulu lakini baadaye akarejea tena kuendelea kuiongoza.
Chanzo: MWANANCHI

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: SERIKALI YAITAJA KAMPUNI YA MANJI ITAKAYOIFUTA KWA KUKIUKA SHERIA
SERIKALI YAITAJA KAMPUNI YA MANJI ITAKAYOIFUTA KWA KUKIUKA SHERIA
https://1.bp.blogspot.com/-NmfngXdIvVs/WZahKj6h8WI/AAAAAAAAdr8/kmLTxFPm8eMLcfyctOgOjW2jvXESIUGxgCLcBGAs/s1600/x00390330-2c4dd8e08d046f465ace43ba6e2fc0aa-arc614x376-w1200-640x375.jpg.pagespeed.ic.ab0nyzNrBV.webp
https://1.bp.blogspot.com/-NmfngXdIvVs/WZahKj6h8WI/AAAAAAAAdr8/kmLTxFPm8eMLcfyctOgOjW2jvXESIUGxgCLcBGAs/s72-c/x00390330-2c4dd8e08d046f465ace43ba6e2fc0aa-arc614x376-w1200-640x375.jpg.pagespeed.ic.ab0nyzNrBV.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/serikali-yaitaja-kampuni-ya-manji.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/serikali-yaitaja-kampuni-ya-manji.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy