SERIKALI YAONGEZA MUDA WAKUNYONYESHA KWA WATUMISHI WENYE WATOTO

SERIKALI imeongeza saa za unyonyeshaji kwa watoto kwa watumishi wa serikali, mashirika pamoja sekta binafsi ili kuwezesha watoto kuwa na afya bora inayotokana na maziwa ya mama.
Hayo ameyasema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akifungua Wiki ya Unyonyeshaji, amesema kuwa mama mzazi baada ya kumaliza miezi mitatu ataingia kazini 3:30 na kuondoka saa 7:30 katika kumuwezesha mama kunyonyesha mtoto bila kuingiliwa na majukumu ya kikazi.
Waziri Ummy amesema kuwa watendaji wa Umma na mashirika pamoja na taasisi lazima wafanye hivyo katika kutambua umuhimu wa mama mzazi kunyonyesha kwa muda uliowekwa kwa kipindi cha miezi sita.
Amesema kuwa ni gharama kubwa katika kuhudumia watoto walio na utapiamlo ambao unatokana moja ni kukosa maziwa ya mama kwa muda mrefu hivyo kuepuka ni njia rahisi ikiwemo kutengwa kwa masaa hayo.
Waziri ameongeza kuwa suala la lishe lazima liangaliwe kwa ukaribu na wadau wote katika kuweza kuwaondoa watoto katika utapiamlo ambao unafanya kudumaa kwa akili.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chakula na Lishe Nchini (TFNC), Joyceline Kaganda amesema jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika juu ya masuala ya lishe na wadau kwa mifumo mbalimbali.
Amesema kuwa wiki ya unyonyeshaji wa kina mama ni muhimu katika katika ukuaji wa mtoto wa kumjenga katika afya bora.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Lishe nchini (Panita), Tumaini Mkindo amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. Pombe Magufuli imwemeka kipaumbele katika ubaoreshaji wa lishe nchini.
Amesema kuwa sera zimeweza kuongezeka katika masuala ya lishe ikiwa eneo la kipaumbele katika mpango wa taifa wa miaka mitano pamoja mikoa na halmashauri kuwa na bajeti ya lishe.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post