SERIKALI YATANGAZA TAREHE YA KULIPIGA MNADA JENGO LA YANGA

Mapema leo asubuhi zimeanza kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha kuwa Jengo la Makao Makuu ya Klabu ya Yanga litapigwa mnada kutokana na deni inalodaiwa.
Taarifa hiyo inayoonyesha kuwa ni tangazo lililotolewa na Kampuni ya Udalali ya Msolopa iliyopewa kibali na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeeleza kwamba jengo hilo litapigwa manada Agosti 19 mwaka huu.
“Wizara ya Ardhi kupitia kwa Kamishna wa Ardhi na kupitia kesi mbalimbali ilizofungua katika Baraza la Ardhi na Nyumba katika Wilaya ya Temeke na Ilala na kushinda, wizara inatangaza mnada wa hadhara kwa tarehe kama inavyoonekana katika jedwali. Minada yote itaongozwa na kusimamiwa na Msolopa Investment Company Ltd,”lilieleza tangazo hilo.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa mwezi Mei mwaka huu alithibitisha kuwa klabu hiyo ilikuwa ikidaiwa na kueleza kuwa uongozi umeanza utaratibu wa kulifanyia kazi suala hilo.
Mkwasa alisema kuwa deni hilo limetokana na malimbikizo ya ada ya jengo la kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo, lakini wanaamini watalilipa kabla ya mchakato huo wa kunadi jengo hilo la makao makuu haujafanyika.
Kama taarifa hizi ambazo hazijathibitishwa na Yanga zitakuwa ni sahihi, ni dhahiri watakuwa hawakulipa deni walilokuwa wakidaiwa ndio sababu wizara ikaamua kulipiga mnada.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post