SHAMSA FORD: MUME WANGU HAWEZI KUOA MKE WA PILI

Msanii wa maigizo nchini Tanzania, Shamsa Ford amesema mume wake Chid Mapenzi hawezi kuoa mke wa pili hata kama dini yake inaruhusu.
Akipiga story na Zote kali muigizaji huyo amesema mume wake hawezi kufanya kitu kama hicho kwasababu hakuna anachokosa kwake.
“Mume wangu kuoa mke wa pili haiwezekani yaani hawezi  kwasababu hana sababu ya kufanya hivyo,” amesema. “Mimi namridhisha kwa kila kitu.  halafu pia mimi mwenyewe nilishawahi kumgusia suala la mke wa pili kwasababu dini yetu inaruhusu, akasema hawezi kwasababu mke wa pili tutaanza kukaribisha mambo ya ushirikina, umaskini na kutokuendelea kimaisha,” amesisitiza.
“Na kama ikija kutokea ndo anataka kuoa  mke wa pili  nataka anipe sababu za kujitosheleza  na ziwe za msingi.”
Shamsa ni mke wa mfanyabiashara huyo ambapo bado hawajabahatika kupata mtoto pamoja.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post