SHULE YAFUNDISHA JINSI YA KUTOA TALAKA- INDIA

Shule moja nchini India itaanza kuwafunza wavulana wa Kiislamu njia za kutoa talaka kulingana na sheriza za Kiislamu.
Shule hiyo iitwayo Dargh-El-Ala Hazrat inayosimamia madrassa 15,000 za Kiislamu ilitangaza kuchukua hatua hiyo baada ya agizo la mahakama lililopiga marufuku talaka za moja kwa moja.
Mtaala wa shule hiyo unaangazia Koran na sharia za kiislamu pamoja na talaka, lakini siyo kwa kina.
‘Tulifanya mkutano wa viongozi wa dini pamoja na wale wa Madrassa baada ya agaizo la mahakama kuu na tumewaelezea jamii kupitia wanafunzi na katika ibada za siku ya Ijumaa kuhusu njia bora za kutoa talaka”, Maulana Shanbudin Racvi kiongozi mkuu wa dini aliambia BBC Hindi.
Aliongeza kuwa hatua hiyo itaeleza vyema kwamba talaka ya moja kwa moja zinazotekelezwa nchini India haziambatani na sharia za kiislamu.
Haijajulikana bado ni vijana wa umri upi (kati ya miaka mitano hadi 16) watakaofunzwa kuhusu talaka.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

SHARE THIS

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post