SUMAYE AFUNGUKA SERIKALI KUMNYANG’ANYA MASHAMBA YAKE

Frederick Sumaye.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye amesema kunyang’anywa mashamba yake si sababu ya yeye kufikiria kurudi CCM.
“Kunyang’anywa mashamba yangu najua ni uamuzi wa juu haunidhoofishi nifikirie  kurudi CCM’’
Sumaye amesema mashamba yaliyofutwa na Serikali yalikuwa yanalipiwa kodi na yalikuwa yanamilikiwa kisheria.
“Wanataka nirudi CCM, mimi sitaki kurudi CCM, kwanini wananilazimisha?  Nilisema sababu za kuondoka huko, waseme wazi sababu za kuyafuta ni za kisiasa tu,” amesema Sumaye leo katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post