TAARIFA KUHUSU KUINGIA NCHINI KWA WAHAMIAJI KUPITIA MPAKA WA KENYA

SHARE:

Zimekuwepo taarifa za kuingia nchini kwa wahamiaji haramu kupitia mpaka wetu na Nchi ya Kenya. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  kupitia ...

Zimekuwepo taarifa za kuingia nchini kwa wahamiaji haramu kupitia mpaka wetu na Nchi ya Kenya. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  kupitia Idara yake ya Uhamiaji inawahakikishia Watanzania kwamba  hatua  kali za kisheria  zinachukuliwa  dhidi  ya raia wote wa kigeni  wanaoingia  nchini kinyume cha  Sheria  za Uhamiaji  na nchi yetu
Kimsingi hakuna raia  yeyote wa kigeni anayeruhusiwa kuingia nchini kwa kisingizio cha  kuja kufanya kazi, biashara au Uwekezaji bila kufuata Sheria  na taratibu za Uhamiaji, na kwamba  wote wanaokiuka  Sheria hizo watarudishwa makwao mara moja.
Ni jambo lisilokubalika mtu atoke nchini kwake bila kibali cha kufanya kazi Tanzania kwa madai kwamba alishatuma maombi ya kibali husika na amekuja kusubiri majibu ya kibali hicho akiwa Tanzania. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi haitavumilia ukiukwaji huu wa sheria za nchi na kwamba kila raia wa kigeni  anayekusudia kuingia nchini ahakikishe ana kibali cha kuingia nchini na anafanya kazi ambayo ndiyo aliyoiombea kwenye kibali chake.
Yapo matukio ya raia wa nchi jirani, hususan katika mipaka ya Kenya na Uganda ambapo kutokana na hali  ya muingiliano  wa kiuchumi na kijamii, raia  wa nchi zetu, wamekuwa  wakivuka mipaka  pande zote  kufuata huduma mbalimbali, Hii pia inachangiwa na mapungufu katika  usimamizi wa alama na maeneo ya wazi ya mipaka yetu. Hali hii inapelekea baadhi ya wananchi wetu kutumia mwanya huo kuwatengenezea  raia  wa kigeni mazingira ya kuingia nchini bila  kufuata taratibu au hata kutumiwa katika biashara haramu ya kusafirisha  binadamu.
Tahadhari inatolewa kwa Watanzania wote ambao wamekuwa wakiwapokea raia hao  wa kigeni na kuwahifadhi, kwani kufanya hivyo  ni kuvunja  sheria za nchi ikiwemo ile Sheria  ya usafirishaji  haramu wa binadamu.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara yake ya Uhamiaji imeanza kuchukua hatua ili kuweza kushughulikia suala hili. Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna Makakala, tayari ametembelea baadhi ya maeneo ya mipaka yetu hususani kijiji cha Jasini wilayani Mkinga mkoani Tanga ili kujionea hali halisi na kutoa Maelekezo ya hatua  za kuchukua  kudhibiti hali hiyo kwa mujibu wa Sheria, kwa kuwa eneo hilo linaonyesha kuwa na muingilino baina ya nchi ya Kenya na Tanzania kwa muda mrefu.
Wizara itaendelea na Mashauriano na Mamlaka nyingine zenye dhamana ya Kusimamia alama za mipaka ya nchi yetu kwa kuwa tatizo hili la muingiliano wa wananchi wa pande zote lipo kwenye mipaka mingi ya nchi.

Imetolewa na
Christina R. Mwangosi
Kaimu Msemaji
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
4 Agosti 2017

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: TAARIFA KUHUSU KUINGIA NCHINI KWA WAHAMIAJI KUPITIA MPAKA WA KENYA
TAARIFA KUHUSU KUINGIA NCHINI KWA WAHAMIAJI KUPITIA MPAKA WA KENYA
https://2.bp.blogspot.com/-X1KT14ZMbQI/WYVb6EK4azI/AAAAAAAAdR4/UnzZDuc1nAEhiK7Pnu_5EGdIp5u-bh5EgCLcBGAs/s1600/x385346719-750x375.jpg.pagespeed.ic.7R5ofH5UaK.webp
https://2.bp.blogspot.com/-X1KT14ZMbQI/WYVb6EK4azI/AAAAAAAAdR4/UnzZDuc1nAEhiK7Pnu_5EGdIp5u-bh5EgCLcBGAs/s72-c/x385346719-750x375.jpg.pagespeed.ic.7R5ofH5UaK.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/taarifa-kuhusu-kuingia-nchini-kwa.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/taarifa-kuhusu-kuingia-nchini-kwa.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy