TAARIFA MUHIMU KWA WAOMBAJI WOTE WA MIKOPO YA VYUO VIKUU 2017/18

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa siku saba wa kutuma maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 ili kutoa nafasi kwa waombaji mikopo ambao hawajakamilisha baadhi ya hatua za kujaza fomu za maombi kukamilisha na kutuma.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bodi ya Mikopo zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji Bw. Abdul-Razaq Badru amesema kuwa maombi ya mikopo yaliyokuwa yafungwe Septemba 4, yataendelea hadi Septemba 11, 2017.
Aidha, Badru amewasisitiza waombaji wa mikopo kuzingatia mwongozo uliotolewa na Bodi unaowataka kuambatanisha nyaraka zote zilizothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamimi (RITA), makamishina wa viapo, mawakili na serikali za mtaa na kuziwasilisha kwenye mtandao wa Bodi.
Maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018, yanayofanyika kwa njia ya mtandao olas.heslb.go.tz  yalifunguliwa Agosti 6, 2017.
Mpaka kufikia Agosti 29, 2017, maombi ya mkopo zaidi ya 50,000 yalikuwa yametumwa Bodi ya Mikopo kwa ajili ya uhakiki na baadaye kupangiwa mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post