TAARIFA MUHIMU KWA WOTE WALIOOMBA NA WATAKAOOMBA KAZI SERIKALI

SHARE:

Mtakumbuka Serikali katika mwaka wa fedha uliomalizika  2016/2017  iliahidi kutoa Ajira serikalini zaidi ya  52,000  kwa Watanzania, amba...

Mtakumbuka Serikali katika mwaka wa fedha uliomalizika 2016/2017 iliahidi kutoa Ajira serikalini zaidi ya 52,000 kwa Watanzania, ambapo katika siku za hivi karibuni Serikali imekuwa ikitoa vibali vya kuajiriwa watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo Waalimu wa Sayansi, Kada za Afya na maeneo mengine kulingana na mahitaji.
Kama mnavyofahamu mojawapo ya jukumu la msingi la kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni pamoja na kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya waajiri mbalimbali na hatimae kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi wanaofaulu usaili, ambapo tangu Serikali ilipoanza kutoa vibali baada ya kusitishwa tumeshapokea jumla ya vibali kwa ajili ya mamlaka za Ajira 239, kati ya hivyo vipo ambavyo vimeshafanyiwa kazi na vingine mchakato wake unaendelea katika hatua mbalimbali.
Aidha, baadhi ya vibali ambavyo mchakato wake umeshakamilika ni pamoja na  kibali cha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambayo tulipokea jumla ya  maombi ya kazi 6,852 na walioitwa kwenye usaili kutokana na kukidhi vigezo  walikuwa  2,949, kwa upande wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) maombi yaliyopokelewa ni  9,022 na walioitwa kwenye  usaili ni  1,550. Aidha, miongoni mwa taasisi ambazo mchakato wake bado unaendelea ni pamoja na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili  (MUHAS) ambapo jumla ya maombi ya kazi 2,273 yamepokelewa na waliokidhi vigezo vya kuitwa kwenye usaili ni 144,  maombi yaliyopokelewa kwa ajili ya Wakala wa Serikali Mtandao (e-GA),yalikuwa 5,732 na  walioitwa kwenye usaili ni 4,054. Taasisi nyingine ambayo mchakato wake unaendelea ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo ina nafasi wazi za kazi 400 na jumla ya maombi ya kazi 56,815 yamepokelewa kupitia mfumo wa uwasilishaji wa maombi ya kazi kwa njia ya kielektroniki “Recruitment Portal’ na baada ya kufanyiwa kazi waliokidhi vigezo kwa mujibu wa sifa zilizokuwa zimeainishwa katika tangazo la kazi husika na kuitwa kwenye usaili ni 29,674.
Pamoja na nia ya Serikali ya awamu ya tano kuendelea kuhakikisha Watanzania wanaohitimu katika fani mbalimbali ndani na nje ya nchi wanapata kazi, zipo changamoto kadhaa ambazo zimekuwa zikijitokeza wakati wa utekelezaji wa mchakato wa ajira ambazo hupelekea baadhi ya waombaji kazi kutoitwa kwenye usaili. Kama mlivyoona katika takwimu zilizoainishwa hapo juu katika baadhi ya taasisi ambazo mchakato wake umeshafanyiwa kazi kupitia Sekretarieti ya Ajira.
Aidha, tungependa mzifahamu changamoto hizo ili mtusaidie kuendelea kuelimisha wadau wetu tukitambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuelimisha na kuhabarisha jamii  ili nao waweze kuzifahamu, kuzielewa na kuzifanyia kazi ili nafasi nyingine za kazi zitapotangazwa waweze kuziepuka na kuwa katika nafasi nzuri na uhakika wa kuweza kuitwa kwenye usaili na hatimae kupata kazi wanazoomba.
Changamoto hizo ni pamoja na Waombaji wengi kutokufahamu namna ya kuandika barua za maombi ya kazi, kutoainisha nafasi wanazoomba, kutokusaini barua za maombi ya kazi wanazoziwasilisha, kutokuthibitisha nyaraka zao (certify) katika wanavyotakiwa kufanya hivyo, hususan kwa waombaji waliosoma nje ya nchi kutowasilisha vyeti vyao vya elimu kwa ajili ya uthibitisho wa kutambulika elimu walizozipata katika mamlaka husika kama NECTA, NACTE na TCU kabla ya kuzituma Sekretarieti ya Ajira.
Sambamba na hizo, ni baadhi ya waombaji kutokuambatisha nyaraka za elimu hususani cheti cha kidato cha nne na sita au astashahada, stashahada, shahada, shahada ya uzamili na kuendelea kulingana na elimu waliyonayo. Baadhi yao kutozingatia vigezo vya nafasi iliyotangazwa, ikiwemo kudanganya sifa wakidai wamemaliza shahada ya fani fulani ilihali hawajasoma shahada ya aina hiyo, au mwombaji mwenye elimu ya astashahada kuomba kazi ya shahada, kuandika barua moja ya kuombea kazi kwa nafasi tofauti, kutojua namna ya kuandika wasifu binafsi  (CV), waombaji wengi kuandika wadhamini wachache ambao ni ndugu zao badala ya idadi ya wadhamini inayotakiwa ambao wanauwezo wa kutoa taarifa zao za kitaaluma na kikazi kwa uhuru pindi wanapotakiwa kufanya hivyo.
Changamoto nyingine ni baadhi ya waombaji kazi wanapoelekezwa kuwasilisha picha za utambulisho wao “Pasportsize” wao wanapakia kwenye mfumo picha tofauti bila kujali mavazi wanayovaa, mandhari iliyotumika na aina za picha wanazotuma. Changamoto nyingine ni ya baadhi ya waombaji kazi ambao ni Waajiriwa katika Utumishi wa Umma kutokupitisha barua za maombi yao kwa Waajiri wao kabla ya kuziwasilisha Sekretarieti ya Ajira, pamoja na baadhi ya waombaji kuja kwenye usaili wa mchujo au mahojiano bila ya vyeti vyao halisi kama inavyoelekezwa.
Nyingine ni  waombaji wengi kutozingatia masharti ya jumla ikiwemo, kuwasilisha nyaraka pungufu mfano kutokuwasilisha barua ya maombi ya kazi, kutokuambatisha baadhi ya vyeti vya taaluma, kuwasilisha maombi, kwa njia tofauti na ile iliyoelekezwa kwenye tangazo la kazi,  kuwasilisha taarifa za uongo mfano, wasifu binafsi usio wa ukweli, kutopakia taarifa sahihi (upload) katika maeneo husika ya mfumo wa kuombea kazi pamoja na kupakia vyeti visivyokamilika mfano “result slips, partial transcript, provisional result, progress report, statement of result”.
Tumeainisha baadhi ya mapungufu hayo hapo juu ili wahitimu ambao ni waajiriwa watarajiwa wafahamu hivi sasa soko la ajira ni la ushindani mkubwa na linahitaji mwombaji aliyejiandaa vizuri. Tunaamini endapo muombaji yeyote wa kazi mwenye sifa na ambaye anazingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali kwenye maombi ya kazi anayowasilisha ataitwa kwenye usaili. Kwakuwa wale ambao wahazingatii kikamilifu mara nyingi hukosa fursa ya kuitwa katika usaili na kuikosa nafasi anayotarajia na hatimae  kusababisha malalamiko.
Aidha, ni vizuri wakafahamu Serikali inatumia gharama kubwa katika kuendesha mchakato wa Ajira hadi kukamilika, na ni nia ya Serikali kuona kila nafasi inayotangazwa inapata mwombaji makini mwenye sifa, ujuzi na weledi wa kutosha kuweza kutumikia Taifa lake. Mwisho, nimalizie kwa kutoa rai kwa waombaji kazi wote wanaomba kazi serikalini kujiandaa kikamilifu pamoja na kuzingatia masharti ya matangazo husika kwa kuhakikisha wanaambatanisha nyaraka zinazotakiwa na kuomba nafasi za kazi ambazo wana sifa stahiki. Niwaahidi kuwa Sekretarieti ya Ajira itaendelea kutoa elimu zaidi na kuwataka wale wenye changamoto ambazo wanaona wanahitaji msaada wasisite kuwasiliana na taasisi kwa kufika katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira au kupitia mawasiliano yetu katika mitandao ya kijamii kama facebook.com/sekretarietiajira, twitter.com/psrsajira, instagram:psrsajira au kwa simu za kiganjani kupitia namba 0784398259/0687624975.
Imetolewa na; Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, tarehe 24 AGOSTI, 2017.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: TAARIFA MUHIMU KWA WOTE WALIOOMBA NA WATAKAOOMBA KAZI SERIKALI
TAARIFA MUHIMU KWA WOTE WALIOOMBA NA WATAKAOOMBA KAZI SERIKALI
https://2.bp.blogspot.com/-eLJ9O6pRf8Q/WZ_TV5M6wRI/AAAAAAAAd80/DXyzzySK47g2VGxh3OQTD4roY73K_0BMACLcBGAs/s1600/xemployment_application-300x200.jpg-750x375.jpg.pagespeed.ic.DWsB5SwxYB.webp
https://2.bp.blogspot.com/-eLJ9O6pRf8Q/WZ_TV5M6wRI/AAAAAAAAd80/DXyzzySK47g2VGxh3OQTD4roY73K_0BMACLcBGAs/s72-c/xemployment_application-300x200.jpg-750x375.jpg.pagespeed.ic.DWsB5SwxYB.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/taarifa-muhimu-kwa-wote-walioomba-na.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/taarifa-muhimu-kwa-wote-walioomba-na.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy