TANZANIA YASHINDA NA KUWA NCHI BORA ZAIDI KWA UTALII AFRIKA 2017

Mtandao wa safaribookings.com wa nchini Uholanzi imefanya uchunguzi na upembuzi wa kina katika nchi mbalimbali za Afrika ili kuweza kujua nchi ambayo ndiyo kituo bora cha utalii kwa mwaka 2017.
Katika uchunguzi huo, Tanzania imeibuka kuwa kituo bora cha utalii Afrika kwa mwaka 2017 huku ikifuatiwa na Zambia na Botswana.
Machapisho zaidi ya 2,500 yalitumika katika uchunguzi huo. Ushirikiano mwingine ulipatikana kutoka watalii kutoka maeneo mbalimbali dunia.
Nyaraka nyingine zilipatikana kutoka kwa waandishi maarufu wa vitabu vya kuongozea watalii kama Lonely Planet, Rough Guides, Frommer’s, Bradt and Footprint ambao pia ni watalaamu kutoka SafariBookings.
Mtandao huu ulifanya uchunguzi kama huu mwaka 2013 ambapo Tanzania iliibuka mshindi. Kwa kipindi cha muda mrefu hawakufanya tena utafiti sababu ya mambo kubadilika, lakini jambo ambalo halijabadilika ni ubora wa Tanzania.
Baadhi ya waliohojiwa walisema kuwa, Tanzania ni bora kutokana na uwepo wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Bonde la Ngorongoro (Ngorongoro Creater). Wengine walisema Tanzania kuna wanyama wa aina mbalimbali, lakini pia huduma zinazotolewa kwa watalii ni bora zaidi Afrika.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post