TAZAMA MUONEKANO WA OFISI YA RAIS TRUMP IKIWA HAINA VITI NA MEZA (SAMANI)

Kitu kimoja ambacho huenda hukudhani kama ungeweza kukiona karibuni ni ofisi ya Rais wa Marekani maarufu Oval Office ikiwa haina samani za ndani.
Ofisi hiyo ambayo ipo ndani ya Ikulu ya Marekani ndiyo hutumiwa kwa shughuli za rais na sasa unaweza kuiona ikiwa tupu bila kiti, meza, makochi, picha au kitu kingine ambacho umewahi kukiona kutokana na ukarabati mkubwa unaoendelea.
Afisi ya Trump ikiwa bila fanicha
Ukarabati huu umetajwa kuwa ni mkubwa zaidi kuwahi kufanyika ndani ya kipindi cha miongo 6 iliyopita.
Wakati ukarabati ukiendelea, Rais wa Marekani Donald Trump yupo mapumziko katika klabu yake ya gofu katika Jimbo la New Jersey, ambapo alichukua likizo ya siku 17.
Jengo hilo linalofahamika kama West Wing ndipo wasaidizi wa Rais pia hukaa, mikutano ya kimataifa hufanyika na mambo mengine nyeti kwa taifa la Marekani.
Hapa chini ni picha nyingine za ukarabati huo.
Nyaya zinaonekana katika eneo ambalo meza ya Trump kawaida huwaNyaya zinaonekana katika eneo ambalo meza ya Rais wa Marekani huwa inawekwa.
Mitambo ya kiyoyozi, ambayo iliwekwa miaka 27 iliyopita, inabadilishwaMitambo ya kiyoyozi, ambayo iliwekwa miaka 27 iliyopita, inabadilishwaworkers dig up pavementa worker fixes windows

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post