TUNDU LISSU APEWA ONYO LA MWISHO NA MAHAKAMA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuonya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa kutofika mahakamani mara mbili.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa alitoa onyo hilo baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Kishenyi Mutalemwa kudai kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa mshtaka lakini mshtakiwa hakuwapo.
“Ni rai ya upande wa Jamhuri kwamba Mahakama iukumbushe upande wa utetezi kuwa mshtakiwa Lissu ni wakili mzoefu na kwamba utaratibu wa kuomba udhuru mahakamani unafahamika na uzingatiwe,” alisema.
Hakimu Mwambapa alisema kwamba hiyo ni mara ya pili kwa Lissu kutofika mahakamani kuhudhuria kesi yake ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni Julai 10, 2017 na mara ya pili ni jana.
Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya alidai kuwa imetokea bahati mbaya, lakini Hakimu Mwambapa alimueleza kuwa mfululizo wa bahati mbaya haukubaliki na akatoa onyo la mwisho.
Jamhuri iliomba kesi hiyo ipangwe tarehe ya karibu kwa ajili ya kusikilizwa na Mahakama ilikubali na kupanga iendelee kwa kusikilizwa Agosti 22 mwaka huu.
Lissu anakabiliwa na kesi ya uchochezi ikidaiwa kuwa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alisema:
Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya udikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote.
“Huyu dikteta uchwara lazima apingwe kila sehemu. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga, nchi itaingia ndani ya giza nene.” Kauli hizi alizotoa lisu ndio zinazompandisha kizimbani zikidaiwa kuwa ni za kichochezi.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post