UAMUZI WA MAHAKAMA KUHUSU KESI YA MANJI YA DAWA ZA KULEVYA

Leo Agosti 25, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kuwa mfanyabiashara Yusuf Manji ana kesi ya kujibu katika shtaka la matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroine linalomkabili.
Akitoa uamuzi huo mahakamani hapo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha, amesema kuwa baada ya mashahidi wa upande wa jamhuri kuwasilisha ushahidi wao mbele ya mahakama, amejiridhisha kuwa mtuhumiwa huyo anayo kesi ya kujibu.
Mkeha amesema kuwa, Yusufu Manji ambaye pia ni Diwani wa CCM katika Kata ya Mbagala vipimo vya pili vilivyofanyika kwenye mkojo wa Manji vimeonyesha kuna dawa aina ya Morphine ambayo metaboli ya heroine.
Akitoa ushahidi wake mahakamani hapo juzi, Mkemia Dominican Dominic alifafanua kuwa, ni vigumu kupata heroine ndani ya mkojo kwani inapokuwa ndani ya mwili kwa dakika 20 hadi 60 hubadilishwa na kuwa morphine.
Baada ya kupatikana na kesi ya kujibu ya matumizi ya dawa za kulevya, Manji atatakiwa kujitetea mbele ya mahakama ambapo wakili wake, Hudson Ndusyepo alisema mshtakiwa atajitete kwa hati ya kiapo ambapo watakuwa na mashaidi 15.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 30 na 31 mwaka huu itakaposikilizwa kwa siku zote mbili.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post