UAMUZI WA WABUNGE WALIOVULIWA UANACHAMA CUF KUTOLEWA LEO

Baada ya Jaji Lugano Mwandambo wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kutupilia mbali kwa mara ya kwanza maombi ya waliokuwa wabunge nane wa CUF walioitaka Mahakama kulizuia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutowaapisha wabunge wateule kutokana na kuwapo kwa mapungufu ya kisheria, Jaji huyo anatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho leo.
Wabunge wateule waliowekewa zuio la kuapishwa ni Rukia Ahmed Kassim, Shamsia Aziz Mtamba, Kiza Hussein Mayeye, Zainab Mndolwa Amir, Hindu Hamis Mwenda, Sonia Juma Magogo, Alfredina Apolinary Kahigi na Nuru Awadh Bafadhili.
Jaji Mwandambo atatoa uamuzi kuhusu zuio lililowekwa kutaka wabunge wateule nane walioteuliwa hivi karibuni kutoapishwa kushika nyadhifa zao. Uamuzi huu utatolewa baada ya Mahakama kusikiliza hoja ya pande zote mbili zinazopingana ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) kuhusu maombi ya wabunge 8 na madiwani wawili wa chama hicho waliofukuzwa uanachama.
Katika maombi ya zuio hilo, wabunge nane wa CUF (waliofukuzwa uanachama hivyo kupoteza ubunge wao) waliiomba Mahakama hiyo kuweka zuio la Wabunge hao kutoapishwa kushika nyadhifa zao hadi kesi yao ya kupinga kufukuzwa uanachama itakapoamuliwa.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post