UFAFANUZI KUHUSU FAINI ZA TANROADS, SUMATRA NA POLISI

SHARE:

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazozua mkanganyiko kwenye mitandao ya kijamii kuhusu faini zinazotoshwa na Wakala wa Usi...

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazozua mkanganyiko kwenye mitandao ya kijamii kuhusu faini zinazotoshwa na Wakala wa Usimamizi wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa madereva wanaozidisha mwendo wa magari au kufanya makosa mengine ya barabarani.
Kufuatia mkanganyiko huo, Balozi wa Usalama Barabarani (RSA) ambao hujitolea kutoa elimu ya usalama barabarani kuhakikisha watumiaji wote wa barabara wanakuwa salama.
Katika ufafanuzi huo uliotolewa na RSA, kwanza walianza kujibu swali ambalo liliulizwa na wengi kama TANROADS ina mamlaka ya kupiga faini kwa kosa la mwendokasi.
TANROADS kama mamlaka ya usimamizi wa barabara chini ya Sheria ya Barabara (ROADS ACT 2007) inayo mamlaka ya kuwaadhibu wale wote wanaokiuka mwendo uliooneshwa kwenye alama za barabarani au kadiri ya maelekezo yao.
Mamlaka haya wanayapata kwa mujibu wa kifungu cha 32(2) cha Sheria ya Barabara, Na.13 ya mwaka 2007. Hata hivyo, ili mtu atozwe faini chini ya sheria hiyo ni hadi atiwe hatiani.
Inayotia mtu hatiani ni mahakama, hivyo ukikamatwa na TANROADS unatakiwa kufikishwa mahakamani na huko ukipatikana na hatia uweze kutozwa kiasi cha shilingi 200,000 au jela mwaka 1, na sio vinginevyo.
Jambo jingine lilitotolewa ufafanuzi baada ya kuzua maswali ni kama kweli faini za barabarani zinazotozwa kwa kosa la mwendokasi sasa ni sh 200,000 na inagawanyika mara tatu yaani kiasi cha shilingi 90,000 kinaenda SUMATRA, Shilingi 30,000 kinaenda Polisi na inayobaki ni ya TANROADS.
RSA wameeleza kwamba, madai hayo ni upotoshaji. Faini ya chini ya sheria ya barabara ni shilingi 200,000 kwa kuzidisha mwendo kinyume na kifungu cha 32(2) na haigawanyiki.
“Haiwezekani kutozwa faini zaidi ya moja kwa kosa hilo hilo. Kwani sheria inasema mtu hataadhibiwa mara mbili kwa kosa hilo hilo alilolitenda mara moja. Iwapo mtu ameadhibiwa mara mbili adhabu hiyo ya pili ni batili. Ndio kusema kwamba, hata mamlaka zote 3 ziwepo pamoja, ukikamatwa umezidisha mwendo utaadhibiwa mara moja tu na mamlaka ile iliyokukamata.”
Mabalozi hao walilazimika kulielezea hilo baada ya kuwepo swali kama inawezekana mtu mmoja akaadhibiwa na mamlaka zote tatu kwa pamoja endapo zitakuwa barabarani kwa wakati mmoja eneo moja zinafanya operesheni.
Kuhusu uwepo wa sheria 3 kwa jambo hilo hilo moja la kuzidisha mwendo, imeelezwa kwamba kila sheria ilitungwa kipindi tofauti na nyingine na kila sheria inasimamiwa na mamlaka yake bila mamlaka moja kuiingilia nyingine.
SUMATRA anasimamia Transport licensing Act Cap 317 na kanuni zake, ambapo faini ni kati ya shilingi 200,000 na 500,000. TANROADS inasimamia Roads Act 2007 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009, ambapo faini ni shilingi 200,000 huku Polisi wakisimamia Sheria ya Usalama Barabarani (Road Traffic Act Cap 168) ambapo faini yake ya papo kwa papo ni shilingi 30,000 bila kujali ukubwa au udogo wa kosa.
Kila mamlaka inasimamia sheria yake na kwamba mamlaka moja mfano Polisi hawawezi kukuandika faini kwa kutumia sheria ya TANROADS. Kama watataka kufanya hivyo watalazimika kukukabidhi kwa mamlaka hiyo.
Washirikishe na wenzako waweze kupata elimu ya usalama barabarani.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: UFAFANUZI KUHUSU FAINI ZA TANROADS, SUMATRA NA POLISI
UFAFANUZI KUHUSU FAINI ZA TANROADS, SUMATRA NA POLISI
https://2.bp.blogspot.com/-lQ43IMbJIbM/WZc4umXNBKI/AAAAAAAAdtE/UkdP8kF_TlINFubU1vIaDSHVcOnUDkAPwCLcBGAs/s1600/xDHffoWMU0AEtkWB-750x375.jpg.pagespeed.ic.7NssLtzS7g.webp
https://2.bp.blogspot.com/-lQ43IMbJIbM/WZc4umXNBKI/AAAAAAAAdtE/UkdP8kF_TlINFubU1vIaDSHVcOnUDkAPwCLcBGAs/s72-c/xDHffoWMU0AEtkWB-750x375.jpg.pagespeed.ic.7NssLtzS7g.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/ufafanuzi-kuhusu-faini-za-tanroads.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/ufafanuzi-kuhusu-faini-za-tanroads.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy