UFAHAMU MPANGILIO WA VYEO VYA JESHI LA POLISI TANZANIA

Kesho Agosti 25 Jeshi la Polisi Tanzania (Tanganyika wakati huo) litatimiza miaka 98 tangu liliponzanishwa kwa mara ya kwanza na wakoloni wa Kiingereza. Jeshi hilo lilinzishwa Agosti 25 mwaka 1919 ambapo makao yake makuu yalikuwa Lushoto mkoani Tanga.
Lengo kubwa la jeshi hilo wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa kutumikia maslahi ya wakoloni ambapo lilitumika katika kuhakikisha shughuli za wakoloni zinakwenda sawia pamoja na kuahakikisha usalama wao.
Baada ya kupata uhuru mwaka 1961, lengo la jeshi hilo lilibadilika kutoka kutumikia watawala na badala yake likawa linawatumikia wananchi kwa kuhakikisha ulinzi na usalama wao pamoja na mali zao lakini kuhakikisha pia wananchi wanafuata sheria.
Kuhusu mpangilio wa vye vya jeshi hilo, kuna ngazi 15 ambapo ngazi ya juu kabisa ni Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) na ngazi ya chini kabisa ni Konstebo wa Polisi (pc).
Kila Askari Polisi ambaye yupo katika ngazi fulani, huwa na alama begani mwake ambayo huonyesha ngazi aliyopo ili kurahisisha utambulisho wakati wowote.
Hapa chini ni mpangilo wa vyeo vya Jeshi la Polisi Tanzania;
 1. Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP)
 2. Kamishina wa Polisi(CP)
 3. Naibu Kamishina wa Polisi(DCP)
 4. Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP)
 5. Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP)
 6. Mrakibu Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SSP)
 7. Mrakibu wa Polisi(SP)
 8. Mrakibu Msaidizi wa Polisi(ASP)
 9. Mkaguzi wa Polisi(Insp)
 10. Mkaguzi Msaidizi wa Polisi(A/Insp)
 11. Sajini Meja wa polisi(rsm)
 12. Stesheni Sajini wa Polisi(s/sgt)
 13. Sajini wa Polisi(sgt)
 14. Koplo wa Polisi(cpl)
 15. Konstebo wa Polisi(pc)
Kwa picha, hizi ni alama ambazo huwa mabegani wa mwa Polisi kuashiria ngazi zao ndani ya jeshi hilo;
Tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania mwaka 1964, Jeshi la Polisi Tanzania limekuwa na Ispekta Jenerali  wa Polisi 10. Kwa majina yao ni, Elangwa N. Shaidi (1964 – 1970), Hamza Azizi (1970 – 1973), Samweli H. Pundugu (7/8/1973 – Aug 1975), Philemon N. Mgaya (8/8/1975 – Nov 1980).
Wengine ni, Solomoni Liani (2/11/1980 – 30/11/1984), Harun G. Mahundi (1/12/1984 – 3/5/1996), Omar I. Mahita (4/5/1996 – 2/3/2006), Saidi A. Mwema (3/3/2006 – 30/12/2013), Ernest J. Mangu (01/01/2014-29/05/2017) na Simon Nyakoro Sirro (29/05/2017-Hadi Sasa).
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post