UGOMVI WA DIAMOND, ALIKIBA NA OMMY DIMPOZ WAVUKA MIPAKA

Ugomvi wa Diamond na Alikiba na Ommy Dimapoz unaweza ukawa umevuka mipaka baada ya mama mzazi wa Diamond kuingizwa katika mgogoro huo, kwa namna inayoonekana ni kumkosea heshima.
Baadhi ya watu wamemkosoa Ommy Dimpoz kwa kuweka picha yake akiwa na mama Diamond katika ukurasa wake wa Instagram huku akitoa maelezo yanayoonyesha kwamba yeye ndio baba mzazi wa Diamond.
Ujumbe uliowekwa na Ommy Dimpoz unasomeka;
BARUA YA WAZI KWA BINTI YANGU MALKIA WA NGUVU
Baadhi ya watu waliokwetwa na ujumbe huo ni pamoja na aliyekuwa Meneja wa Ommy Dimpoza, Mubenga ambapo ameandika akimtaka msanii huyo kuacha kuwaheshimu wazazi na kama ameshindwa mziki basi akae pembeni.
Omary mdogo wangu maandiko yanasema waheshimu wazazi upate heri na Miaka mingi duniani na mzazi sio mpaka akuzae ata mzazi wa mwenzio pia ni mzazi wako why unamuingiza mama naseb kwenye mambo yenu? Uko ni kukosa adabu wew si unajifanyaga innocent kwa watu kumbe una pretend? Wew sindio uliyeimba nani kama mama imekuwaje leo una watusi wa kina mama? Au ndio stress za Mziki? Watu wanataka video ya cheche na sio kutusi wazazi wa watu usituaribie muziki wetu kama game imekushinda please kaa pembeni pia naomba vyama vyenye dhamana ya muziki vichukue atua kali zidi ya matusi ya omary kwa mama wa diamond ili iwe fundisho kwa wengine ya kwangu ni hayo tu! 
Mbali na Mubenga watumiaji wengine wa mitandao ya kijamii wamekerwa na kitendo hicho cha Ommy Dimpoza huku wakimtaka kutoingiza wazazi kwenye ugomvi wao binafsi.
Kutokuelewana huko kati ya Diamond na wasanii wenzake wawili Ommy Dimpoz na Alikiba kumetokana na wao kuwaimba vibaya katika wimbo wa Fresh Remix.


JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post