UTATA KESI YA MANJI, MKEMIA HAJUI ALIPIMA MKOJO WA NANI

Sina uhakika na hiyo sampuli ya mkojo niliyoletewa ambayo niliipa namba ya usajili 367/2017 kama ni ya Yusuf Manji au ni ya Askari aliyeenda naye chooni.
Kauli hiyo ilizua utata na mshangao jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya kutolewa na Mkemia Dominican Dominic kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati alipokuwa akitoa ushahidi katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Yusuf Manji.
Dominic alijibu hivyo baada ya kuulizwa na wakili anayemuwakilisha Manji, Hudson Ndusyepo kama anaweza kusema huo mkojo alioupima ni wa Yusuf Manji au Askari aliyeingia naye chooni.
Alipoulizwa kama wakati wa kuchukua sampuli ya mkojo wa Manji na yeye alikuwepo, shahidi huyo alisema aliandaa mazingira na kukabidhi kikontena kidogo kwa Askari Sospeter wakati wa uchukuaji wa sampuli. “Nilikuwa nje nasubiri, Manji na Askari huyo waliingia chooni ili atoe sampuli na akatoa.”
Dominic ambaye ni shahidi namba tatu katika kesi ya matumizi ya heroine inayomkabili Diwani wa Mbagala, Yusuf Manji akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Cyprian Mkeha alisema uchunguzi wa awali alioufanya kwenye sampuli ya mkojo huo alikuta una dawa  aina ya benzodiazepines.
Sahidi huyo aliiambia mahakama kuwa kwa uzoefu wake na uchunguzi ambao amewahi kuufanya alisema kuwa, mtumiaji anayetumia dawa hiyo iliyokutwa kwenye mkojo, mara nyingi hutumia heroine au cocaine.
Katika uchunguzi mwingine aliofanya kwa kutumia mashine ya HPLS, Dominic alisema ulionyesha una dawa aina ya morphine ambayo ni metaboli (metabolites) ya heroine. Alifafanua mahakamani hapo kuwa ni vigumu kupata heroine ndani ya mkojo kwani inapokuwa ndani ya mwili kwa dakika 20 hadi 60 hubadilishwa na kuwa morphine.
Shahidi huyo alisema dawa aina ya benzodiazepines iliyokutwa kwenye mkojo aliopima alisema hutumika hospitalini kutuliza maumivu makali au kumpatia mtu usingizi.
Baada ya wakili kufunga ushahidi huo, Hakimu Mkeha alisema kwamba atatoa uamuzi kesho endapo mtuhumiwa huyo ana kesi ya kujibu ama la.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post