VIDEO: MKE WA ROMA AELEZA SABABU ZA NDUGU KUTOONEKANA WAKATI MUMEWE AMETEKWA

Mke wa Rapa ROMA Mkatoliki ameweka wazi alivyokutana na Roma kwa mara ya kwanza, walivyoanza uhusiano wao na hadi kufikia wawili hao kuamua kufunga ndoa.
Nancy pia alieleza sakata zima la kutekwa kwa ROMA lilivyoathiri familia yao na kisa cha ndugu zake ROMA au yeye kutokuonekana kwenye harakati za kumtafuta ROMA.
Hayo yote aliyasema alipokuwa akifanya mahojiano katika kituo cha runinga cha East Africa Tv wakati akitambulisha wimbo mpya wa mumewe ambapo alieleza kwamba si kweli ndugu zake au ndugu wa mumewe hawakuwepo pamoja nao katika kipindi kigumu walichopitia.
Ndugu zangu na ndugu wa mume wangu walikuwa pamoja nasi katika kipindi chote ila wasingeweza kuja mbele hadi waonekane kwenye vyombo vya habari. Na mara nyingi wasanii ndio nilikuwa nashirikiana nao, naonekana kwenye vyombo vya habari, lakini wao pia walikuwepo sema tu kwa vile hawakuonekana, alisema Nancy.
Hapa chini ni mahojiano yote aliyofanya FNL.JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post