VITA YA ‘VIEWS’ YOUTUBE… ROMA KICHWA NGUMU

R.O.M.A Mkatoliki.
VIDEO kutazamwa na watu wengi kwenye Mtandao wa YouTube ni suala la kujivunia kwa wanamuziki wengi duniani hivi sasa. Ndiyo maana mwanamuziki Luis Fonsi baada ya wimbo wake uitwao Despacitoaliomshirikisha Daddy Yankee kutazamwa na watu zaidi ya bilioni 3.4, karibia nusu ya watu duniani, amevunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Wiz Khalifa na wimbo wa See You Again ambao Umetazamwa na watu wasiyozidi bilioni 3.1 mpaka Jumapili ya juzi..
Ushindani kimuziki umefi kia huko kwa sasa.
Ambapo Bongo timu mbalimbali zimekuwa zikiundwa na wanamuziki ili kuhakikisha wanapotoa kazi zinawafi kia watumiaji wa mitandao wapatao milioni 9.7 Tanzania, hii ni kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na kugonga views nyingi YouTube.
Tumeona siku za hivi karibuni wanamuziki mbalimbali wametoa ngoma mpya zilizoambatana na video. Video kali ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa wa kugombea ‘airtime’ kwenye media.
Miongoni mwawanamuziki waliotoa video ni Joh Makini- Kata Leta, R.O.M.A wimbo uitwao Zimbabwe, Fid Q- Fresh, Aslay- Pusha, Jux- Utaniua na Alikiba wimbo uitwao Seduce Me.
Kati ya wanamuziki hawa wote na wengine ambao hawajaorodheshwa ni Kiba ndiye aliyekimbiza kwa views. Amekuwa mwanamuziki wa kwanza kwenye historia ya muziki Afrika Mashariki kugonga views zaidi ya milioni 1.8 mpaka jana (Jumatatu).
Anayemfuata ni R.o.m.a na wimbo wake wa Zimbwabwe ulioangaliwa na watu zaidi milioni 1.2 pia huku Joh Makini na Kata Leta yake akiwa na views mpaka sasa zisizozidi laki 6.
Fresh wa Fid Q unachezea kwenye laki mbili na Aslay yeye hadi juzi Jumapili alikuwa yumo kwenye laki moja.
Katika listi ya wanamuziki wa Hip Hop, R.O.M.A ndiye mwanamuzi pekee ambaye ameweza kuonesha kuwa ni kichwa ngumu kwa kukimbizana na kina Kiba.
Roma ameonesha kuwa ana nguvu ya watu. Ingawa wimbo wa Kiba hauna zaidi ya siku nne , umeupita wake wenye takribani wiki tatu lakini takwimu zinaonesha R.O.M.A ni zaidi ya wanamuziki wa Hi Hop Bongo kupata views nyingi YouTube.
Amewazidi Joh Makini ambaye ambaye amefanya wimbo na Davido mwanamuziki mwenye jina kubwa duniani kwa sasa na Fid Q mwenye heshima kubwa kwenye tasnia ya muziki Bongo!
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post