VITU VINNE UNAVYOTAKIWA KUWA NAVYO KWENYE GARI ILI USIKAMATWE NA POLISI

SHARE:

Ni jambo zuri wakati wote kuhakikisha kwamba chombo chako cha usafiri kinakuwa katika mpangilio unaotakiwa ili kuepuka usumbufu unaoweza ...

Ni jambo zuri wakati wote kuhakikisha kwamba chombo chako cha usafiri kinakuwa katika mpangilio unaotakiwa ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza barabarani mfano kukamatwa na Polisi wa Kikosi cha Usalama barabara.
Polisi wanapokukamata hufanya ukaguzi kuhakikisha kuwa gari lako linakuwa salama linapotumia barabara ili usipate ajali na hata ukipata uweze kudhibiti madhara yake. Lakini ukaguzi huo hulenga pia kuhakikisha kwamba gari lako haliwi chanzo cha ajali za barabarani.
Katika makala hii, tutachabua kwa undani vitu vinne muhimu sana unavyotakiwa kuwa navyo kwenye gari wakati wowote ili kuepuka kumatwa na Polisi na kufkishwa mahakamani au kutozwa faini.
Kwanza, kabla ya kuaza safari hakikisha kwamba gari lako lina kifaa cha kuzimia moto (Fire extinguisher). Mungu apitishe mbali, fikiri unaendesha gari na kutokana na sababu yoyote ile gari linaanza kuwaka moto ghafla. Je! Ni hatua gani utachukua kuhakikisha unadhibiti madhara ya moto huo?
Unapokuwa na mtungi wenye gesi ya Carbondioxide au Sodium bicarbonate katika gari lako, utakurahisishia kuzima moto huo na hivyo kuliokoa gari lako na kuteketa kwa moto. Lakini pia utaweza kuepusha madhara yanayoweza kupata magari mengine yaliyopo pembeni au vitu vyako vya thamani ndani ya gari.
Endapo unatakuwa huna kifaa hiki ndani ya gari, Polisi watakutoza faini na kutakiwa kununua kwa ajili ya kudhibiti moto. Mitungi hii si mikubwa, ni midogo ili kuwezesha kubebwa kwa urahisi.
Image result for Car Fire extinguisher
Pili, unatakiwa kuwa na ‘Reflector’ muda wote katika gari lako. Fikiri kwamba umepata matatizo ya gari, ni usiku na pengine labda umepata tatizo kwenye kona, utawezaje kuweka kiashiria ili gari jingine likija ajue mbele kuna tatizo?
Reflector ambapo wengine huziita triangle kutokana na kuwa na umbo la pembe tatu hutumika kutoa ishara kwa madereva wengine kuwa, mbele kuna gari limepata tatizo hivyo awe makini. Kifaa hiki huakisi mwanga, hivyo kinapomulikwa na taa za gari jingine hungaa zaidi kutoa ishara.
Licha ya kuwa magari mengine huwa na reflector ilipo taa ya breki, lakini Polisi hutaka uwe na nyingine kwa sababu reflector iliyopo kwenye taa za gari haitompa muda wa kutosha dereva wa chombo kingine cha usafiri kufanya maamuzi sahihi kwani atashtukia gari likiwa karibu.
Baadhi ya watu wamekuwa wakilalamika kuwa reflector zao huibwa wanapoziweka barabarani, lakini hilo halitoi uhalali wa kutokuwa nayo kwenye gari.
Image result for Triangle reflector car night
Kitu kingine unachohitajika kuwa nacho mara zote unapokuwa kwenye gari ni leseni ya udereva. Polisi huhitaji kila dereva awe na leseni ya udereva ili kujiridhisha kuwa amefuzu vigezo na ana elimu ya matumizi ya barabara ndio sababu akaaminiwa na kupewa kibali cha kuendesha gari.
Ikumbukwe kuwa, hapa sio kwamba utahitajika kuwa na leseni tu, bali leseni hiyo iwe halali. Miongoni mwa vitu vinavyoifanya leseni yako kuwa halali ni pamoja na iwe ndani ya muda wake wa matumizi, uwe unaendesha chombo cha moto ambacho kimeruhusiwa na leseni yako.
Polisi anapokukamata na kutaka kukuandikia faini, hasa kwa kutumia mfumo wa kielektroniki, huhitaji leseni yako ili kuweza kuchukua namba zilizopo pale. Hata hivyo, unapokamatwa ukiwa hauna leseni, utapewa saa 72 (siku 3) kuiwasilisha leseni yako katika Kituo cha Polisi.
Kitu cha mwisho lakini si kwa umuhimu unachotakiwa kiwa nacho kila mara unapotumia gari lako ni kadi ya gari. Kadi ya gari ni muhimu kuwa nayo wakati wote kwa sababu hiyo ndiyo yenye maelezo yote kuhusu gari lako.
Kadi ya gari imesheheni maelezo ya gari kuanzia namba ya gari, rangi, aina, muundo, ukubwa wa injini, usajili, mmiliki na vitu vingine vingi muhimu. Polisi anapokusimamisha, huhitaji kukagua kadi ya gari ili kujirishisha kuwa, maelezo yaliyopo kwenye kadi yako, yanaendana na chombo unachoendesha.
Kama unaona tatizo kutambea na kadi ya gari kwa hofu kwamba huenda ukaipoteza, unaweza kuidurufisha kisha ukawa unatembea na nakala ya kadi.
Image result for Kadi ya gari
Hakikisha unalikagua gari lako vizuri kabisa ili kujiridhisha kama liko sawa kwa safari. Kutumia chombo chochote ambacho hakipo salama, si hatari kwa Polisi aliyepewa jukumu la kusimamia usalama barabarani, bali kwako wewe na watumiaji wengine wa barabara.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: VITU VINNE UNAVYOTAKIWA KUWA NAVYO KWENYE GARI ILI USIKAMATWE NA POLISI
VITU VINNE UNAVYOTAKIWA KUWA NAVYO KWENYE GARI ILI USIKAMATWE NA POLISI
https://1.bp.blogspot.com/-zHGGd9ZkZmQ/WZRx1Bt0RLI/AAAAAAAAdk8/uym5xQkb0EYEymBzXwTFXeaZTu4p7q8lACLcBGAs/s1600/x5R5A0408-750x375.jpg.pagespeed.ic.AsXCAcuQeh.webp
https://1.bp.blogspot.com/-zHGGd9ZkZmQ/WZRx1Bt0RLI/AAAAAAAAdk8/uym5xQkb0EYEymBzXwTFXeaZTu4p7q8lACLcBGAs/s72-c/x5R5A0408-750x375.jpg.pagespeed.ic.AsXCAcuQeh.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/vitu-vinne-unavyotakiwa-kuwa-navyo.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/vitu-vinne-unavyotakiwa-kuwa-navyo.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy