VIWANDA NANE WALIVYONYANG’ANYWA WAMILIKI KWA AGIZO LA RAIS

Siku chache baada ya Rais Dkt Magufuli kutangaza hadharani kuwa haridhishwi na utendaji kazi wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage kutokana na kumualika kufungua viwanda tu lakini hasikii habari za watu kunyanganywa viwanda, waziri huyo ametangaza uamuzi wa serikali kuvitwaa kutoka mikononi mwa wawekezaji walioshindwa kuviendelea viwanda nane.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Waziri Mwijage alisema kwamba serikali imeanza mchakato wa kuvichukua viwanda hivyo baada ya kufanywa uchunguzi na kubaini kuwa mikataba ya mauzo ya viwanda hivyo imekiukwa.
Viwanda vilivyotwaliwa na serikali ni, Kiwanda cha Korosho (Lindi), Mgodi wa Pugu Kaolin, Mkata Saw Mills Limited, Manawa Ginnery Co Ltd, Dabada Tea Factory, Tembo Chipboard Ltd, Kilimanjaro Textile Mills na Mang’ula Michanical and Machine Tools Co Ltd.
Akitangaza uamuzi huo, Waziri alisema kuwa mmiliki wa viwanda vya serikali ni Msajili wa Hazina na hivyo wamiliki wa viwanda hivi watatakiwa kuvilinda hadi hapo watakapofanya makabidhiano na serikali.
Aidha, waziri aliwataka watanzania na wanafunzi wanaomaliza vyuo mbalimbali nchini kuchangamkia fursa hizo za kuwekeza kwenye viwanda ili kuweza kutengeneza ajira lakini pia kufanikisha lengo la kufikia Tanzania ya Viwanda.
Pia waziri aliwataka watu wote ambao wamebinasishiwa viwanda na serikali kuwasiliana na serikali wanapopata changamoto yoyote kuviendesha lakini pia hata wanapotaka kubadilisha matumizi ya kiwanda, mfano kuzalisha biadhaa nyingine tofauti na ya awali, lazima wawasiliane na serikali ili ifahamike bidhaa gani inazalishwa wapi.
Akieleza hali ya viwanda kwa sasa nchini, Waziri Mwijage alisema kwamba, viwanda vinavyofanyakazi vizuri ni 62, vinavyofanyakazi kwa kusuasua ni 28, vilivyofungwa ni 56 na vilivyobinafsishwa kwa kuuza mali moja kwa moja ni 10.
Kuhusu hivyo 56 vilivyofungwa alisema, kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za kubaini hali halisi ya viwanda hivyo ambapo wanachambua mkataba wa mauzo ili kuainisha vifungu vya uwajibikaji kwa kila upande.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post