WAFUNGWA WENYE MIMBA MAREKANI HUFUNGWA MIKONO NA MIGUU WAKIWA WANAJIFUNGUA

Watu wengi wanashangazwa jinsi wafungwa wa kike wanavyofanyiwa magerezani na kwamba inabidi mfumo mzima uzingatiwe ubinadamu wa mtu, hata kama ni mfungwa anayehitaji kurekebishwa. Ingawa wafungwa wa kike wanakumbwa na changamoto nyingi, moja ya mambo ya kushangaza kwenye magereza ya nchini Marekani ni kitendo cha kuwafunga wanawake wajawazito wakati wakijifungua magerezani.
Muswada uliowasilishwa mwezi Julai unaotaka kuzuiwa kwa kuwafunga wafungwa wakati wa kujifungua na kuhakikisha maisha mazuri kwa wafungwa wa kike kwa ujumla. Muswada huo unapendekeza wafungwa hao wapatiwe huduma za kupiga simu bure, baruapepe na simu ya Skype kati ya wafungwa hao na familia zao zilizopo uraiani, kuitaka mamlaka ya magereza kufikiria ni wapi pa kuwaweka watoto wa wafungwa hao na kutaka wafungwa wa kike wapate vitambaa vya kujisitiri vya bure wakiwa magerezani.
Ingawa takwimu sahihi za wafungwa wenye mimba hazipo, takwimu za mwanzoni mwa miaka ya 2000 zinaonesha kwamba takribani asilimia 3 ya wafungwa wa kike huingia kwenye magereza ya Serikali kuu wakiwa na mimba, na kwa wale wanaoingia kwenye magereza ya majimbo, asilimia 4 huwa na mimba, na asilimia 5 ya wanawake wanaofungwa kwenye magereza ya vitongoji huingia magerezani humo wakiwa na mimba. Takwimu za hivi karibuni zilizochapishwa kwenye jarida la Chama cha Uhuru wa Raia nchini Marekani (ACLU) zinaonesha kuwa kwa wafungwa wa kike zaidi ya 200,000 wanaoingia magerezani kila mwaka, takribani asilimia 6 (watu 12,000) wanaingia gerezani wakiwa na mimba. Kuwafunga wafungwa wanaojifungua ni jambo la kisheria kwa zaidi ya nusu ya majimbo ya nchi hiyo.
Kuwafunga pingu na minyororo wafungwa wanaojifungua ni moja tu ya matatizo makubwa wanayopata wafungwa wa kike kwenye magereza nchini Marekani. Mambo kama umaskini, jinsia na rangi na kwa wafungwa — hasa wenye watoto — yana athari kubwa sana.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post