WAKODIWA KWA SHILINGI LAKI TANO KUMUUA DEREVA BODABODA

Watu watatu wamefikishwa mbele ya Jaji Mfawidhi Mwanaisha Kwariko wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kwa madai ya mauaji ya muendesha pikipiki, Bahati Masawe waliotekeleza tukio hilo baada ya kuahidiwa shilingi laki tano, televisheni na redio ya sabufa.
Wakili wa Serikali aliwasomea maelezo ya awali na kusema kuwa washtakiwa Petro Gabriel, Abel Ezekiel na Manase Lazaro (wote wakazi wa Wilaya ya Mkalama) walifanya mauaji hayo tarehe 1/02/2016 kwa kumnyonga Masawe na kumtumbukiza kwenye kisima cha majitaka cha kijiji cha Ishenga, Wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Alisema marehemu alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu (Abel) akimtaka aende kumchukua na kumpeleka kijiji cha Ibaga wilayani Mkalama. Wakiwa njiani alijitokeza mtu mwingine ambaye ni mshtakiwa namba moja (Petro), na walipofikia mbali kidogo, walimsimamisha na kufanya tukio hilo la mauaji.
Alisema kuwa washtakiwa baada ya kufanya mauaji hayo na kutumbukiza mwili wa marehemu Bahati kwenye kisima cha maji, walitokomea na pikipiki hiyo. Februari 26 mwaka 2016, baba wa marehemu alipata taarifa kuwa pikipiki ya mwanaye ipo Katesh mkoani Manyara, akiwa nayo mshtakiwa Petro.
Baba wa marehemu alitoa taarifa polisi, na baada ya Petro kukamatwa alieleza kuwa ni kweli walimuua Bahati kwa kukodiwa na Manase.
Wakili huyo alisema kuwa baada ya kuhojiwa, Petro alisema kuwa Manase aliwaahidi kuwapatia shilingi laki tano, televisheni pamoja na redio ya sabufa wakifanikiwa kumuua na kumpelekea pikipiki hiyo. Hata hivyo, hakumkabidhi pikipiki hiyo Manase kwakuwa hakuwa na fedha aliyowaahidi na kulazimika kubaki na pikipiki huku wakitafuta mteja wa kuinunua.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post