WANANCHI WA BUNDA WAMTAKA BULAYA AMSHTAKI WASIRA

Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya, amewaomba wananchi kuamua iwapo ni sahihi yeye kumfungulia kesi ya madai ya fidia kudai gharama za kesi aliyofunguliwa kupinga matokeo na Mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Stephen Wasira katika mkutano ambao alisema lengo lake ni kuwapa taarifa wananchi juu ya kesi ya kupinga matokeo ya ubunge iliyokuwapo na tukio la yeye kufukuzwa bungeni.
Alisema kuwa kwa miaka miwili alishindwa kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na kesi ambayo ilikuwa ikiendelea lakini kwa sasa imemalizika na kilichobaki ni kushughulikia kuwaletea maendeleo wananchi ambao walimchagua kufanya hivyo.
Mbunge huyo aliwauliza wananchi iwapo wanataka amfungulie kesi ya madai ya fidia na wananchi walipaza sauti kwenye mkutano huo uliofanyika kituo cha zamani cha mabasi kuwa amfungulie kudai fidia, ambapo kwa sauti ya juu kabisa walikubaliana na wazo hilo.
“Kama wananchi mmenikubalia nimdai fidia ya gharama ya kesi ya uchaguzi basi nitawasiliana na Wakili Tundu Lissu aandae taratibu za kufungua kesi ya fidia tuweze kudai, na fedha atakayolipa nitaielekeza kwenye shughuli za maendeleo,” alisema Bulaya.
“Nawashukuru wananchi kwa kipindi chote cha miaka miwili ambayo mzee Wasira na watu wake walikuwa wakipambana niweze kuvuliwa ubunge. Ameshindwa mara tano kuanzia kura zetu hadi kwenye Mahakama alipokuwa amekimbilia.
“Hivi karibuni tumemshinda kwenye Mahakama ya Rufaa na tunayo nafasi ya kudai fidia ya gharama za kesi kwa kipindi chote kesi ilivyokuwa ikiendelea,” alisema Bulaya.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post