WANAODAIWA RAIA WA RWANDA WASHAMBULIA MSAFARA WA MKUU WA WILAYA WA KARAGWE

Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheluka akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya wameshambuliwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za jadi.
Tukio hilo lilitoke jana Agosti 29, wakati kiongozi huyo alipokuwa katika walipowasili katika Kijiji cha Kashanda kutatua mgogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Katika shambulio hilo, Diwani wa Kata ya Nyakahanga, Charles Bechumila amejeruhiwa kwa mshale na kukatwa na panga baada ya kuanguka alipokuwa akikimbia katika hali ya kujihami dhidi ya watu hao.
Kufuatia kelele za kuomba msaada za kiongozi huyo, Polisi waliokuwa wameandamana nao walilazimika kufyatua risasi angani na kisha kuwatawanya watu hao na diwani huyo akakimbizwa katika Hospitali ya Nyakahanga.
“Baada ya kufika eneo lile, tuliwakuta watu wawili wakiendelea na shughuli za kilimo katika eneo lililotengwa kwa ajili ya wafugaji; baada ya msafara kusimama, kuwahoji na kuwatia mbaroni watu hao mishale ilianza kurushwa kutoka vichakani,” alisema mtu mmoja ambaye alikuwa katika msafara huo.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya alisema kuwa watu wawili wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa lakini pia uchunguzi wa kina unaendelea kuweza kuwabaini wote waliohusika.
Ofisa Tarafa wa Bugene, Rozaria Christian amesema watu waliotekeleza tukio hilo wanaonekana walikuwa wamejiandaa. Lakini alisema pia watu wawili waliokamatwa uchunguzi wa awali umebainisha kuwa si raia wa Tanzania na kwamba walitumwa na wenyeji wao.
Maelezo hayo yanaendana na yale ya Mkuu wa Wilaya aliyesema kwamba katika kijiji hicho kuna raia wengi wa Rwanda ambao huingia nchini kinyume na sheria.
Mgogoro wa wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Kashanda umedumu kwa muda mrefu huku kila upande ukidai ni halali kwao kuendesha shughuli zao katika eneo hilo.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post