WASIFU (CV) YA MWANASIASA MKONGWE EDWARD LOWASSA (64)

SHARE:

Jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Edward Lowassa ambaye alizaliwa Agosti 26, 1953 katika Kijiji cha Ngarash, Monduli na ndiye mtoto mk...

Jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Edward Lowassa ambaye alizaliwa Agosti 26, 1953 katika Kijiji cha Ngarash, Monduli na ndiye mtoto mkubwa wa kiume kwa Mzee Ngoyai Lowassa.
Alianza kusoma katika Shule ya Msingi Monduli kati ya mwaka 1961–1967. Kisha akaendelea kwenye Shule ya Sekondari Arusha kwa kidato cha kwanza mpaka cha nne kati ya mwaka 1968 – 1971, kabla ya kumalizia kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Milambo mkoani Tabora mwaka 1972–1973.
Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1974–1977 na kuhitimu Shahada ya Sanaa katika Elimu (B.A Education) na baadae Chuo Kikuu cha Bath Uingereza kwa Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Maendeleo (mwaka 1983–1984).
Baada ya kumaliza chuo kikuu, Lowassa alifanya kazi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa ofisa wa ngazi ya juu kuanzia wilaya, mkoa na baadaye makao makuu kati ya mwaka 1977–1989.
Aliajiriwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC), mwaka 1989–1990.
Lowassa amemuoa Regina na wana watoto watano, wasichana wawili na wavulana watatu. Watoto hao ni Fredrick, Pamella, Adda, Robert na Richard.
MBIO ZA UBUNGE
Lowassa alichaguliwa kuwa Mbunge kupitia kundi la Vijana ndani ya CCM na akashikilia nafasi hiyo kati ya mwaka 1990 hadi 1995 na mwaka 1993 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais (Haki na Mambo ya Bunge), kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ardhi na Makazi akiwa Waziri mwaka 1993–1995.
Kwenye Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi (mwaka 1995), Lowassa alishinda ubunge kwa asilimia 87.3. Alikaa bila uteuzi wowote kwa miaka miwili. Mwaka 1997–2000, Rais Benjamin Mkapa alimteua kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Kuondoa Umasikini).
Kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 aligombea tena ubunge wa Monduli na kushinda kwa mara ya tatu. Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa Maji na Mfugo hadi mwaka 2005.
Kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005, aligombea ubunge na kushinda kwa asilimia 95.6. Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Bunge likamthibitisha kwa kura 312.
Uwaziri mkuu wa Lowassa ulikoma Februari 2008, alipojiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond.
Kamati Maalumu ya Bunge ya watu watano iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe ilisisitiza kuwa Wizara ya Nishati na Madini na Ofisi ya Waziri Mkuu ndizo zinazopaswa kubeba lawama ya uingiaji wa mkataba mbovu na Richmond, kampuni ambayo uchunguzi ulionyesha kuwa ni ya mfukoni mwa watu huku Serikali ikilazimika kulipa mabilioni ya fedha katika mkataba ambao una upungufu makubwa.
Wakati Lowassa analitaarifu Bunge kuwa amemuandikia Rais barua ya kujiuzulu, alisisitiza kuwa “…anafanya hivyo ili kulinda taswira ya chama chake na Serikali na kuwa shida ya wabaya wake ni u-waziri mkuu na siyo kingine…”
Baada ya kujiuzulu, Lowassa aligombea ubunge kwa mara nyingine Monduli (mwaka 2010) na kupata asilimia 90.93 ya kura zote na hadi sasa ndiye mbunge wa jimbo hili japokuwa amekwishaaga kwamba hatagombea tena kiti hicho.
MBIO ZA URAIS
Lowassa ni miongoni mwa wana CCM 17 waliochukua fomu kuwania urais mwaka 1995 lakini aliyepitishwa ni Mkapa.
Mwaka 2005, hakugombea urais ila alikuwa na mipango ya muda mrefu ya kumsaidia rafiki yake, Kikwete na inadaiwa kuwa makubaliano ya Kikwete na Lowassa yalikuwa kwamba mwenzake akishaongoza nchi kwa miaka 10 (yaani 2005 – 2015) atamtengenezea njia 2015 – 2025.
Tangu Lowassa aachie uwaziri mkuu alianza juhudi zake mwenyewe za kujitengenezea njia ya kuelekea Ikulu na amefanya mambo mengi yanayoashiria kuwa amedhamiria kuingia Magogoni.
Kama kuna mtu nchi hii ametoa michango mingi ya rasilimali fedha katika kuchangia misikiti, makanisa, vijana, vikundi, harambee na vinginevyo, hakuna kama Lowassa. Michango hiyo, wachambuzi wengi waliihusisha na mbio zake za urais.
Baada ya kukatwa katika kura za ndani ya chama ambapo John Pombe Magufuli ndiye alipitishwa, Lowassa aliamua kuhamia CHADEMA ili kuweza kutimiza azma yake ya kuingia Ikulu ambapo huko alipewa nafasi ya kugombea urais.
Akiwa CHADEMA Lowassa aliungwa mkono na UKAWA ambao ni muungano wa vyama vya CHADEMA, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD ambavyo vyote vilikubaliana kuunganisha nguvu na kusimamisha mgombea mmoja ili kuweza kuing’oa CCM madarakani.
Matokeo ya uchaguzi yalimpa ushindi Magufuli na hivyo kuzifuta ndoto za Lowassa kuingia Ikulu kwa mara nyingine.
Baada ya uchaguzi wa 2015 Oktoba, Lowassa alibaki kama mwanachama wa kawaida ndani ya CHADEMA, na baadae aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, nafasi ambayo bado anaishikilia.
Mara kadhaa amekuwa akisikika akisema kwamba atagombea urais kwa mara nyingine katika uchaguzi mkuu wa 2020, lakini chama chake hakijasema lolote kuhusu suala hilo.
-Mtatiro

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,72,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,268,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,11,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,565,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3293,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,332,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,383,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,67,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1376,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1284,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WASIFU (CV) YA MWANASIASA MKONGWE EDWARD LOWASSA (64)
WASIFU (CV) YA MWANASIASA MKONGWE EDWARD LOWASSA (64)
https://2.bp.blogspot.com/-ci7Dm4K8xMM/WaK1iLjQg9I/AAAAAAAAeBk/4NhYuirvvk0otuAv0ala1lvWJVLUj7ZPwCLcBGAs/s1600/xlowassa-mezani-640x375.jpg.pagespeed.ic.y_hLGRFZmY.webp
https://2.bp.blogspot.com/-ci7Dm4K8xMM/WaK1iLjQg9I/AAAAAAAAeBk/4NhYuirvvk0otuAv0ala1lvWJVLUj7ZPwCLcBGAs/s72-c/xlowassa-mezani-640x375.jpg.pagespeed.ic.y_hLGRFZmY.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/wasifu-cv-ya-mwanasiasa-mkongwe-edward.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/wasifu-cv-ya-mwanasiasa-mkongwe-edward.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy