WATOTO WA LUCKY VINCENT WAONDOKA MAREKANI KUJA TANZANIA

Watoto hao wakipanda ndege na wazazi wao.

WATOTO watatu wa Shule ya Msingi Lucky Vincent waliokuwa majeruhi wa ajali iliyotokea Karatu na kwenda kutibiwa nchini Marekani, watawasili kesho asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mjini Arusha.
Watoto hao ambao ni Doreen, Sadia na Wilson waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani tayari wameshapanda ndege kutoka nchini humo kurejea Tanzania baada ya kupata nafuu.
Safari ya kurejea Tanzania ikiwadia.

Watoto hao ni miongoni mwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent walionusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Arusha mwezi Mei mwaka huu, ambapo inakadiriwa idadi ya waliopoteza maisha ni 33 ikijumuisha wanafunzi na walimu waliokuwa katika gari hilo.
Mtandao wa Zote kali blog unawashukuru madaktari na kila aliyetenga muda wake kuwaombea na kuchangia chochote kusaidia matibabu ya watoto hao.
JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Sambaza habari kwa marafiki

Author:

Best Tanzania, Africa and World News Blog, Gossip, Entertainment, Life and Health Tips, Employment and Opportunies,Celebs life and Scandals..... Updated Daily .

Previous Post
Next Post