WAZIRI WA KILIMO AIASA BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO (TADB)

SHARE:

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed ameiasa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuwez...

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed ameiasa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuwezesha wakulima ili waweze kuchangamkia fursa za kuuza mazao ya kilimo nje ya nchi ili kuwaongezea kipato wakulima hao.
Waziri Hamad aliyasema hayo alipolitembelea Banda la TADB katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini humo.
Waziri Hamad alisema kuwa Tanzania inapata fursa nyingi za masoko nje ya nchi kwa mazao mbalimbali ikiwemo zao la karafuu, korosho na mazao ya mikunde ikiwemo dengu na mbaazi zinazotakiwa sana nchini India na Arabuni.
“Naiomba Benki ya Kilimo kuwawezesha wakulima wanaolima kibiashara ili kuchangamkia fursa za masoko kwa mazao ya kimkakati yakiwemo zao la karafuu, korosho na mazao ya mikunde ikiwemo dengu na mbaazi ambazo nchi nyingi marafiki wanahitaji,” alisema Waziri Hamad.
Aliongeza kuwa wizara yake inaletewa maombi mengi ya mazao kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nchi hizo.
Kwa mujibu wa Waziri Hamad kuna wafanyabiashara wa kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu wanaohitaji zaidi ya kontena mbili za korosho kwa wiki hivyo Benki ya Kilimo ina wajibu wa kuwezesha wakulima ili waweze kuchangamkia fursa hizo.
“Naamini Benki ikiwawezesha wakulima wanaweza kuchangamkia fursa za masoko ya nje ikiwemo ya wafanyabiashara kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu wanaohitaji zaidi ya kontena mbili za korosho kwa wiki,” aliongeza.
Akizungumza wakati wa akipokea ugeni huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa TADB ni kuchagiza juhudi za serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania.
Aliongeza kuwa katika kutekeleza hayo Benki ya kilimo imedhamiria na kujizatiti katika kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.
“Lengo letu ni kuhakikisha tuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema Bw. Assenga.
Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa sekta hizo ili kuongeza tija sekta hizo ili kupambana na umaskini nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akiukaribisha ugeni wa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed (kushoto) ulipotembelea Banda la TADB katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini humo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) akizungumza wakati ugeni wa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed (kulia) ulipotembelea Banda la TADB katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini humo.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bw. Simon Migangala (kulia) akieleza machache kuhusu umuhimu wa Benki ya Kilimo kwenye uchumi wa viwanda.
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed (katikati) akizungumza na viongozi wa TADB alipotembelea Banda la TADB katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini humo.
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed akihimiza jambo kwa uongozi wa Benki ya Kilimo.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Sarah V. Chiwamba akizungumza wakati wa Ziara hiyo.
 Hamad akitembelea mabanda ya wakulima walionufaika na Mikopo ya TADB.

COMMENTS

JIUNGE NA ZOTEKALI BLOG
Katika FACEBOOK, TWITTER, INSTAGRAM ili kupata habari zetu kirahisi install app ya ZOTEKALI BLOG HAPA
HTML tutorial

Name

Advertise,33,Afya,73,Beauty,2,Entertaiment,1155,Entertainment,273,EPL,3,Events,4,Fashion,5,Gospel,1,Gossip,13,Hash kinywele,1,Hemed Phd,1,Hemedy Phd,1,Historia,3,Hot kiss,1,Idris Sultan,2,Instagram,1,Interview Questions & Answers,1,Irene,1,Itir Esen,1,Jacqueline Wolper,2,Janet Jackson,1,Jay Maiko,1,Jay Malley,1,Jay z,1,Jaydee,1,Jaygga,1,JB,1,Jishindie,1,Joh Makini,1,Judith Wambura,1,Juma Nature,1,Justin Bieber,1,Jux,1,Kajala Masanja,1,Kala Jeremah,1,Kanye West,2,Kathy Griffin,1,Katuni,18,Kevin Hart,1,Khalighraph Jones,1,Kilimo,7,Kim Kardashian,2,Kimataifa,567,Kiss by Wema,1,Kitaifa,3301,Kukosa Choo,1,Kylie Jenner,1,Lady Jaydee,3,Lee Su Jin,1,Lifestyle,87,Lil Wayne,1,Lulu Diva,3,Mad Ice,1,Madee,2,Magazeti,333,Mahusiano,7,Mai,1,Maimartha Jesse,1,Makala,386,Makomando,1,Malaika,1,Manji,1,Mapenzi,20,Mapishi,2,Mashairi,4,Masogange,1,Mastaa,29,Matonya,1,Matukio,77,Mau Fundi,1,Mc Pilipili,1,mitindo,2,mjamzito,1,Monah,1,Mp3,113,Mr. T Touch,2,Msami,2,Music,346,Mwana FA,1,mwanamke,1,Nafasi za kazi,68,Nahreel,1,Nas B,1,Nash Mc,1,Nay Wa Mitego,6,Nedy Music,2,News,1,Ney Wa Mitego,1,nguvu za kiume,1,Ngwea,1,Nicki Minaj,2,Nikki Wa Pili,1,Nuh Mziwanda,3,nyama ya nguruwe,1,nyusi,1,Ochu,1,Off Shouder Ball Flora Top,1,Ommy Dimpoz,2,Omotola Jalade,1,P The Mc,3,Picha,656,Puff Daddy,1,Q Boy Msafi,3,Quick Rock,1,Quick Rocka,2,Rapper wa Marekani,1,Rayvan,1,Rayvanny,2,Rihanna,2,Rockstar 4000,1,Roma,1,Rummy,1,RunTown,1,Saida Karoli,1,Sauti Sol,1,Selena Gomez,1,Seline,1,Serena Williams,1,Shamfa Ford,1,Shetta,1,Shilole,4,Shishi,1,show kali,1,Siasa,1379,Simba SC,1,Simulizi,1,Smartphone,1,Sports,1286,Stamina,1,Stori kubwa,6,Tangazo,1,Technology,32,Tip Top Connection,1,Tiwa savage,1,Tom Ford,1,Travis Scott,1,Tunda,1,Uchaguzi kenya,1,Uchebe,2,Ucheshi,22,Udaku,49,Umbea,55,Urembo,12,Ushauri,1,Uyee,1,Vera Sidika,2,Video,137,Videos,19,Vitu Amazing,2,VPL,1,Vyakula,1,Wakali Kwanza,1,Wanawake,1,WCB,1,Wema sepetu,8,Witness,1,Wizkid,2,Yamoto Band,1,Young Dee,4,Young Killer,1,Z Anto,1,Zarinah Hassan,1,Zasta,1,Zote kali Tv,132,Zuwena Mohamed,1,
ltr
item
Zotekali Blog: WAZIRI WA KILIMO AIASA BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO (TADB)
WAZIRI WA KILIMO AIASA BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO (TADB)
https://4.bp.blogspot.com/-qZ5w4RupHeQ/WYrOUlKLATI/AAAAAAAAdVE/VTgUP7oTaj04WKs191o8hTp__H4qfOmBgCLcBGAs/s1600/xIMG_0864-750x375.jpg.pagespeed.ic.WW_73WIFEV.webp
https://4.bp.blogspot.com/-qZ5w4RupHeQ/WYrOUlKLATI/AAAAAAAAdVE/VTgUP7oTaj04WKs191o8hTp__H4qfOmBgCLcBGAs/s72-c/xIMG_0864-750x375.jpg.pagespeed.ic.WW_73WIFEV.webp
Zotekali Blog
http://www.zotekali.com/2017/08/waziri-wa-kilimo-aiasa-benki-ya.html
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/
http://www.zotekali.com/2017/08/waziri-wa-kilimo-aiasa-benki-ya.html
true
373551996072538542
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy